MKURUGENZI WA SHIRIKA LA AGRI THAMANI FOUNDATION MH NEEMA LUGANGIRA AONGOZA ZOEZI LA KUGAWA TAULO ZA KIKE WANAFUNZI 1,800 MANISPAA YA BUKOBA

 

 

MKURUGENZI
wa Agri Thamani ambaye Pia ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia NGOs Mh
Neema Lugangira akigawa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule za
Sekondari
WANAFUNZI
wa kike wa shule za Sekondari wakifurahia kupokea mfuko wao uliojaa
taulo za kike za kutosha mwaka mzima kwa kila mmoja
FUSO
lililokuwa limejaa Taulo za kike za wanafunzi wa kike 1800 wa Bukoba
Manispaa likiingia kwenye uwanja wa Kaitaba Bukoba mjini likitokea Dar
es Salaam
Mabox ya Taulo za kike ambazo zote zilikuwa zimeandikwa Jina la Shule ya Sekondari kwa Idadi Kamili ya Wanafunzi wa Kike

Hivi ndivyo kila mwanafunzi wa kike alivyoondoka uwanja wa Kaitaba na Furaha

Mkurugenzi wa Agri Thamani; Mhe Neema Lugangiea (Mb.)
ambae pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) kupitia Kundi la Asasi za
Kiraia (NGOs) Mh.Neema Lugangira ametoa msaada wa taulo za kike kwa
wanafunzi 1800 kutoka kwenye shule 16 za Manispaa ya Bukoba .

 

Ambapo
kila mwanafunzi mmoja ataweza kutumia taulo alizopewa kwa kipindi cha
mwaka mmoja katika zoezi ambalo iliyofanyika kwenye uwanja wa Kaitaba
mjini Bukoba.

Kwa
Manispaa ya Bukoba jumla ya packet 25,200 za Taulo za Kike ziligawiwa
kwa Wanafunzi wa Kike 1,800 kutoka Sekondari 16 za Kata zote 14 za
Manispaa ya Bukoba.


Akizungumza
wakati wa ugawaji wa taulo hizo katika zoezi ambalo liliratibiwa na
Idara ya Elimu Sekondari Bukoba Manispaa na Afisa Elimu Taaluma
Sekondari alishiriki zoezi zima.

 

Mhe
Neema Lugangira amesema ameamua kufanya hivyo ili kuwasaidia wanafunzi
hao kuweza kujihifadhi na kuweza kuendelea na masomo yao wakati wa 
kipindi cha hedhi.

 

Alisema
wanafunzi ambao watanufaika na msaada huo ni kuanzia kidato cha tatu
hadi cha nne ambao kwa sasa wataondoka na adha ambayo walikuwa
wakikumbana nao wakati wakiwe kwenye kipundi cha hedhi.

 

“Naamini
msaada huo utakuwa na manufaa makubwa kwao kutokana na kwamba watatumia
muda mwingi kusoma hata wakiwa kwenye kipindi chao cha hedhi kutokana
na kuwa na taulo ambazo zitawasaidia” Alisema Mbunge huyo.

 

Akizungumzia
kuhusu msaada huo wa Taulo za Kike, Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya
Bukoba Mjini Emanuele Ebeneza alimshukuru Mbunge Neema kwa msaada wake
wa taulo za wasichana ambao utakuwa chachu ya kupunguza utoro shuleni.

 

Alisema
kupitia msaada huo wanafunzi wengi watajua namna ya kujihifadhi na
kupunguza utoro shuleni kwa sababu ya kutokujisikia vizuri kwenye
kipindi cha hedhi.

 

“Niseme
tu kwamba licha ya kutoa msaada huo lakini pia Mbunge Neema anafundisha
wanafunzi juu ya hedhi salama,  anawaandaa kisaikolojia kupita kwenye
kipindi cha hedhi na hivyo kuwaondolea hofu na anawapa elimu ya lishe
bora inayowasaidia waepukane na changamoto ya upungufu wa damu (anemia)
”Alisema Afisa Elimu Sekondari Bukoba Manispaa. 

 

Afisa
Elimu Sekondari huyo alisema kwamba pia Mbunge Neema Lugangira
anawafundisha usafi hatua ambayo inasaidia kupunguza utoro ambao
ungetokana na wanafunzi kushindwa kuhudhuria masomo wakati wa mzunguko
wa hedhi.

 

“Kama
unavyojua mzunguko wa wasichana unatokea kila mwezi mara moja na wakati
mwengine wakishindwa kuhudhuria masomo hivyo alilolifanya ni kitu cha
muhimu sana sana kwa maana ya wanasichana “Alisema Ndg Ebeneza

 

Mmoja
wa wanafunzi hao Alisema kwamba changamoto kubwa ni kubwa pale pedi
zinapokuwa zimekwisha wanashindwa kuishi kwa amani kabisa wakati wakiwa
wanaendelea na masomo

 

Naye
mwanafunzi mwengine amesema wanashukuru kwa msaada huo kutokana na
kwamba wakati mwengine wamekuwa wakikosa shule kutokana na kutokuwa na
taulo za kujihifadhi wakati wakiwa kwenye kipindi cha hedhi.

 

Hata
hivyo Avitha Faustini ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika
Shule ya Sekondari  Hamugumbe alimshukuru Mbunge Neema kwa msaada huo
ambao amewapatia ambao umekuwa ni faraja kubwa kwao na kuwaondolea
changamoto walizokuwa wakikumbana nazo.

 

Alisema
wamepata ujasiri wa kuendele na masomo kwani kabla ya kupata Taulo 
hizo walikuwa wakitokewa na hali hiyo wanakuwa wanyonge na wakati
mwengine hulazimika kurudi nyumbani na  kukosa masomo. Aliongezea kwamba
sasa hivi hawana haja ya kuwaomba wazazi pesa ya kununua pedi.

Mwanafunzi
mwingine alikiri kwamba wengi hawajawahi kuziona taulo za kike na
alielezea njia ambazo wengi wao wanatumia ambazo kwakweli hata sisi
tunashindwa kuziandika maana sio salama kabisa. Mwanafunzi huyu
alionyesha furaha ya aina yake kuona kwamba wamekumbukwa na kuthaminiwa
hata kama wao ni watoto wa kimaskini.

Mradi
huo wa Taulo za Kike umeshawanufaisha  Watoto wa Kike katika mikoa ya
Dodoma, Tabora, Pwani, Tanga, Kigoma, Mtwara na Kagera na mikoa
inayofuata kwa awamu hii ya kwanza ni Ruvuma na Lindi

Mbunge
Neema Lugangira alimalizia kwa kusema kwamba Jumla ya Wanafunzi wa Kike
5,500 nchini watakuwa wamenufika ifikapo mwezi Mei 2021 ambapo Taulo za
Kike zote zimetengenezwa na Kiwanda cha Tanzania ambacho kinauzoefu wa
zaidi ya miaka 40 kwenye eneo hili.
CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )