MKURUGENZI MTENDAJI WILAYA YA BABATI AFARIKI DUNIA.

Na John Walter-Babati
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Babati Hamisi Iddi Malinga amefariki dunia asubuhi ya leo June 14,2020.
Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho Mkuu wa  wilaya ya Babati Elizabeth Kitundu  amesema mkurugenzi Malinga amefariki wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Manyara alipokuwa amelazwa takribani wiki mbili.
Kitundu amesema wilaya ya Babati imepokea kwa masitiko taarifa za msiba huo na kwamba wanashirikiana na  familia kufanya  taratibu za kusafirisha  mwili kwenda Iringa kwa ajili ya Mazishi.
Hamisi Iddi Malinga alikuwa  mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya babati kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka 2020 umauti ulipomfika.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )