MKURUGENZI KAGUNZE ATAJA MIRADI ITAKAYOTEMBELEWA NA MWENGE WA UHURU JULAI 28 MANISPAA YA SHINYANGA

Na
Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkurugenzi
wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze amesema miradi kumi ya
maendeleo itazinduliwa, kufunguliwa na kuwekwa mawe ya msingi na Mwenge wa
uhuru Julai 28, 2023 Mwaka huu.

Amesema maandalizi yamekamilika kwa
asilimia mia moja huku akitaja miradi itakayotembelewa  na Mwenge wa uhuru ikiwa ni pamoja na kupanda
miti, kukagua clabu ya Rushwa na clabu ya lishe katika shule ya sekondari
Rajani kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.

Amesema mwenge wa uhuru utafungua ujenzi
wa madarasa sita (6) na ofisi mbili (2) za walimu katika shule ya msingi
Bugweto na kwamba mradi huo unathamani ya Shilingi Milioni 40.

Mwalimu Kagunze amesema Mwenge wa uhuru
utakagua mradi wa asilimia 10 wa magari mawili ya vijana ya abiria ambapo pia
utafanyika ukaguzi wa shughuli za vijana za usafi na utunzaji wa mazingira,
kushiriki usafi pamoja na kutoa cheti cha pongezi huku akitaja mradi huo
kugharibu zaidi ya Miliani mia moja kwa vijana wa mtaa wa Kalogo kata ya mjini
Manispaa ya Shinyanga.

Mkurugenzi huyo amesema pia utazindua chuo
cha serikali za mitaa kampasi ya Shinyanga kilichopo jingo la SHIRECU ambapo
mradi huo unagharimu  zaidi ya Miliani
mia moja.

Mradi mwingine utakaowekewa jiwe la msingi
ni ujenzi wa madaraja mawili kata ya Kitangili nao unagharibu zaidi ya shilingi
Milioni mia moja pamoja na kuzindua mradi wa maji Bugayambelele kata ya Kizumbi
wenye unaogharimu zaidi ya Milioni mia mbili.

Mwenge huo pia utaweka jiwe la msingi
kwenye ujenzi wa soko la Ibinzamata, kukagua hifadhi ya mazingira NAFRAC
Bushushu kata ya Lubaga, kuzindua mradi wa kiwanda cha maziwa Mwalugoye kata ya
Chibe.

Pia Mwenge wa uhuru utafungua OPD, wodi ya
wazazi, jingo la mionzi na njia za watembea kwa miguu pamoja na kugawa neti,
kukagua upimaji wa malaria na dawa za kulevye katika kituo cha Afya Kambarage
mjini Shinyanga.

Mkurugenzi
wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze amewaomba wakazi wa Manispaa
ya Shinyanga kujitokeza kwa wingi  ambapo
amesema mkesha wa Mwenge wa uhuru 
utafanyika uwanja wa saba saba Kambarage mjini Shinyanga.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )