MEYA TANGA ATAKA HALMASHAURI IWEKWE KWENYE REKODI KWA KUPATA HATI SAFI MIAKA MITATU MFULULIZO

 MSTAHIKI Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapha Selebosi akizungumza wakati wa kikao maalumu
cha Baraza la Madiwani ambacho kilikuwa kikao maalumu cha kupitia na
kujadili hoja za mkaguzi na mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG)kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella na kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji

 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa kikao maalumu
cha Baraza la Madiwani ambacho kilikuwa kikao maalumu cha kupitia na
kujadili hoja za mkaguzi na mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG)kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari na kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapha Selebosi

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari akizungumza wakati wa kikao hicho

 Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji akizungumza wakati wa kikao hicho

 Sehemu ya madiwani wa kata mbalimbali wakifuatilia kikao hicho

 Maafisa kutoka ngazi ya Mkoa wa Tanga wakifuatilia kikao hicho kulia ni Afisa wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga Gipson George

 Sehemu ya wataalamu wa Halmashauri ya Jiji la Tanga wakifuatilia kikao hicho

MSTAHIKI Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapha Selebosi amesema ni muhimu Halmashauri ya Jiji hilo iandike kwenye historia kutokanana na kupata hati safi ya mahesabu miaka mitatu mfululizo huku akieleza hilo limewewezeshwa na mshikamano uliopo katika ufanisi wa kazi .

Huku akieleza hilo limefanikishwa na watendaji wa Halmashauri ya Jiji wakiongozwa na Mkurugenzi Daudi Mayeji ambao wamekuwa wakipambana kuhakikisha mafanikio hayo yanapatikana.

Aliyasema hayo wakati wa kikao maalumu cha Baraza la Madiwani ambacho kilikuwa kikao maalumu cha kupitia na kujadili hoja za mkaguzi na mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) ambapo alimueleza Mkuu wa Mkoa wa Tanga kumfikishia salamu zao Rais Dkt John Magufuli kwa kuitendea haki Halmashauri hiyo kwenye miradi mbalimbali.

“Kwa hili tunafarijika sana kwani Jiji letu limeandika historia kubwa ya kuendelea kupata hati safi mpaka leo hivyo nadhani ingekuwa ni vizuri ingeeandikwa kwenye vitabu ambapo kesho na kesho kutwa watu watambue kwamba viongozi hao walifanya kitu gani”Alisema

Meya huyo alisema kwamba mabaraza yaliyopita walikuwa madiwani tisa wa upinzani lakini mabaraza yalikuwa hayaendi vizuri katika vikao vya halmashauri lakini kwa sasa walikuwepo 20 wa upinzani na 17 wa CCM lakini kwa kuheshimiana wamefanya kazi pamoja bila kujali itikadi za vyama.

“Wakati tunaanza baraza letu tulikuwa na madiwani 20 wa upinzania na 17 CCM lakini kwa kuheshimiana tumefanya kazi pamoja bila kujali itikadi za vyama kwa lengo la kuitanguliza tanga mbele kuheshimiana pekee bali ni utulivu wa Mkurugenzi wa Jiji Daudi Mayeji na Wetandaji wake na hii ni historia haijawahi kuandikwa “Alisema

Hata hivyo Meya huyo alimpongeza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kwa kuwa kiunganishi kikubwa cha maendeleo kwenye Halmashauri hiyo kwa kuwasilisha kero zinazowakabili na hivyo kupatiwa ufumbuzi haraka.

“Kwa kweli Waziri Ummy amekuwa msaada mkubwa sana kwetu kwani kabla hajaingia bungeni anakupigia simu anaachukua taarifa za halmashauri na hivyo hatua hiyo imekuwa chachu kubwa kwa maendeleo ya Jiji hilo na sisi kama tutaendelea kushirikiana naye na kumsapoti”Alisema Meya.

Awali akizungumza wakati wa kikao hicho Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari alisema kwamba makusanyo ya Halamshauri hiyo kuwa asilimia 76 sio mbaya lakini wanatakiwa kujitahidi vyanzo ambavyo vimeorodheshwa hapo ni vingi na vile ambavyo vimepitishwa karibuni wavisimamie kwa ukaribu.

Alisema huo ushuru wa madini,taka ngumu ,nyumba za kulala wageni ikiwemo mazao mbalimbali na mifugo vyote wavisimamie kwa karibu kwa wakati kuhakikisha wanakusanya kodi ili kuweza kutimiza malengo yao na la pili ni upande wa kuangalia mapato bado yapo mikononi mwa wakusanyaji ambayo bado hayajaingia kwenye mfumo na benki .

Hata hivyo aliwaomba wasimamie na kuweka muda maalumu ili fedha ziilingizwe kwenye akaunti na zinaweza kuongeza mapato ya Jiji

Kwa upande wake MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella aliipongeza Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa kupata hati safi na hilo linatokana na usimamizi imara ambao umekuwa mfano wa kuigwa katika maeneo mengine.

Mwisho.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )