Mbunge wa Viti Maalum Kupitia Kundi la Vijana Mhe Mariam Ditopile Leo ametimiza ahadi yake na kukabidhi vifaa Mbalimbali vya Michezo kwa Timu ya UVCCM Wilaya ya Temeke

Mhe Mariam amesema anafurahishwa Sana Namna Timu ya Umoja wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Temeke inafanya Vizuri kwenye Mashindano Mbalimbali ikiwemo kuwa Mabingwa wa Ndondo Cup.

Mhe Mbunge amekabidhi Seti Mbili za Jezi na Mipira Minne na kutoa Kiasi cha Fedha Tasilimu Laki Mbili kwa Vijana wa Hamasa wa Wilaya ya Temeke pia amehaidi Kuwanunulia Sare za Kikundi Hicho ambacho kinaongoza kwa Hamasa Wilaya ya Temeke na Mkoa wa Dar es salaam.

Pia Amewataka Vijana kuendelea kuunga mkono Jitihada za Mhe.Rais Dr John Pombe Magufuli na Kujitokeza kwa Wingi Kushiriki Uchaguzi Mkuu kwa Kugombea nafasi mbalimbali za Udiwani na Ubunge na Kushiriki kwa Kumpigia Kura Nyingi za Kishindo Rais Dkt John Pombe Magufuli.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )