MBUNGE WA VIJANA LUCY JOHN SABU ATEMA CHECHE BUNGENI KUHUSU VIJANA

“Nitoe Rai kwa serikali kuja na mkakati mpya wa kuwasaidia vijana hawa hususani kwa kutoa elimu na mafunzo ya Ujasiriamali”

“Fedha za halmashauri ziingie kwenye hii benki ambayo itakua kila halmashauri itawezesha Vijana kukopa uko. Fedha za mfuko wa maendeleo ya Vijana pia ziingie kwenye benki hii, itatoa mikopo maalumu kwa ajili ya Vijana pekee.”

“Benki ya Vijana ni Muhimu sasa kuanzishwa kwasasa ambayo itakua bank maalumu kwa Vijana kwenda kukopa fedha. kutokana na mifuko 18 ya uwezeshwaji kiuchumi iliyopo ofisi ya Waziri mkuu fedha hizi ziingie moja kwa moja katika Benki”

“Hotuba ya Rais imeeleza mambo mengi ambayo yametoa dira na vipaumbele vya serikali, ambayo imewapa watanzania matumaini makubwa sana hususani kwenye sekta mbalimbali endapo  tulioaminiwa kuwa wawakilishi wa wananchi wenzetu tutafanya kazi kwa bidii, kumsaidia Rais wetu”

“Lengo la serikali kuwawezesha  vijana litafanikiwa endapo tutaendelea kuwajengea uwezo vijana, kwa mfano 4% zitolewazo na Halmashauri, baadhi ya vijana huchukua pasipo kuwa na elimu ya kutosha namna ya kuendesha biashara wanazopanga kuzifanya,”

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )