MBUNGE SUMA FYANDOMO, AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUTOKOMEZA VIFO VYA UZAZI

Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Suma Fyandomo. 

Na Mwandishi Wetu, Rungwe 

WILAYA ya Rungwe mkoani Mbeya imemshukuru Rais
Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kufanikisha mapambano ya vifo vitokanavyo
na uzazi pingmizi, ambapo katika hospitali ya wilaya wanawake zaidi ya 350
wanajifungua kwa mwezi wakiwa salama na watoto.

Uongozi wa wilaya hiyo akiwemo Mbunge wa Viti
Maalum (CCM) Suma Fyandomo, amesema katika mapambano hayo ya vifo vitokanavyo
na uzazi wanamtambua Rais Samia kama askari namba moja mkoani humo kutokana na
uimarishaji wa huduma za afya  ikiwemo upatikanaji wa uhakika wa vifaa.                        

Akizungumza jana katika Hospitali ya Wilaya ya
Rungwe mkoani humo Suma amesema wanamshukuru Rais Dk.Samia kwa kuendelea
kufanikisha mapambano ya vifo vitokanavyo na uzazi pingamizi ambapo katika
hospitali ya wilaya wanawake zaidi ya 350 wanajifungua kwa mwezi wakiwa salama
wao na watoto.

Alisema katika mapambano hayo wanamtambua Rais
Dk.Samia kama shujaa na askari namba moja aliyedhamilia kupunguza vifo
vitokanavyo na uzazi nchini.

“Mkoa huu ni kati ya mikoa ambayo watu
wanazaliana kwa wingi na hapo awali huduma za afya hususani za uzazi zilikuwa
ni changamoto katika vituo na hospitali zetu lakini kwa sasa hususani miaka
miwili hii ya Rais Dk.Samia tumeona uthubutu na uchungu alionao kwa wanawake
wenzie ambapo vifaa tiba na mazingira wezeshe ya klujifungulia yanatuma uhakika
wa kuwapo kwa uzazi salama,”alisema.

Suma alieleza kuwa,katika hospitali hiyo
wanajifungua wanawake zaidi ya 350 
kwa  mwezi na wote wanakuwa salama
na watoto.

Alisema, kwa namna ambavyo uongozi wa Rais
Dk.Samia unamjali mama na motto maboresho ya wodi za kujifunmgua yamezingatia
upatikanaji wa vifaa vyote vya afya vya kisasa kutoka Bohari ya Dawa (MSD)
katika vituo vyote hadi vya pembezoni ambapo kwa sasa wanafanya upasuaji.

“Kuanzia Kyela,Chunya, Mbaral, Mbeya mjini na
Vijijini hakuna maha;li kuna malalamiko ya kukosa dawa na vifaa tiba hadi ngazi
ya zahanati kuna majengo ya kisasa ikiwemo ya huduma za dharula ambapo ujezi
unaendelea kila sehemu , nami katika kuunga mkono jitihada hizo nimenunua  mashuka, viti mwendo kutoka MSD,” alisema.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri  Wilaya ya Rungwe Dk.Diocles Ngaiza alisema katika
idara ya afya maboresho yamekuwa yakiendelea ambapo  mwaka 202/23 na kufungua vituo vya afya
viwili vya Ndanto na Kyimo ambavyo vimepokea mil. 500 kila kimoja na vimeanza
kutoa huduma  vikiwa na vipaumbele ya
huduma ya afya na mama na mtoto kwa maelekezo ya Rais Samia na serikali yake
lengo ni kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi wilayani humo.

“Pia vipo vituo vya afya vingine viwili
vinaendelea kujengwa kikiwemo cha Iponjora ambapo tulipokea milioni 500 ujenzi
upo katika hatua za mwisho na kituo cha Kinyala ujenzi unaendelea kwa fedha za
mapato ya ndani vyote vimelenga kuboresha huduma ya mama na moto,”alisema.

Dk.Ngaiza alisisitiza kuwa,mbali na maboresho
hayo  ujenzi wa ghorofa unaendelea katika
hospitali ya wilaya ambapo wamepokea sh bilioni moja  kwa mwaka wa fedha uliopita na matarajio ni
kupata bilioni moja nyingine kutoa wizarani kuweza kukamilisha ujenzi huo ambao
utahusisha wodi za wagonjkwa wan nje,wa ndani, wodi za mama na mtoto.

Alisema upande wa vifaa tiba kwa mwaka wa 2022/23
wamepokea sh. milioni 400 kwa ajili ya vifaa tiba ambavyo vimefungwa katika
vituo na huduma zinaendelea huku katika bajeti ya mwaka huu idara ya afya
imetenmgewa sh . bilioni 2.8 zitakazonunua vifaa tiba vya sh. milioni 700 na
bilioni moja nyingine ya ujenzi wa vituo vipya viwili vya afya.

“Kipekee idara ya afya imepewa kipaumbele
tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita na Bohari yetu kwa kuwa hizi dawa na
vifaa tiba vyote vinatoka MSD  na
upatikanaji wa dawa katika wilaya hii ni asilimia 92, nishukuru sana uongozi wa
taasisi hiyo Mbeya hivi karibuni nilipeleka ombi la kupatiwa mashine kubwa ya
dawa ya usingizi ilikuwa haipo walipambana imefika hivyo muda wowote
tutaanzisha upasuaji katika kituo cha afya cha Kimo,”alisema.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )