MBUNGE MHE. KATAMBI ATOA ZAWADI YA NAFAKA NA VITOEO KWA KAMATI YA SIASA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA NA MKOA WA SHINYANGA.

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Naibu
waziri ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal
Patrobas ametoa zawadi ya nafaka  na
vitoweo mbalimbali baada ya kufurahishwa na kazi zinazofanywa na viongozi wa Wilaya na Mkoa wa Shinyanga  ikiwemo kamati ya siasa pamoja na kamati ya ulinza na
usalama.

Mhe. Paschal Patrobas Katambi ameipongeza
kamati ya siasa kupitia chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga  kwa
kuendelea kutekeleza vyema majukumu yao wakishirikiana na kamati ya ulinzi na
usalama katika kuimarisha amani Wilaya na Mkoa wa Shinyanga kwa ujumla.

Ametoa zawadi ya Ng’ombe wawili (2),
kuku kumi (10) pamoja na kilo 200 za mchele huku akikemea suala la ukatili
unaoendelea kufanyika kwenye jamii katika Mkoa wa Shinyanga.

Amesema Mkoa wa Shinyanga ni miongoni
mwa Mikoa yenye amani na utulivu katika masuala ya kisiasa ambapo amewaoma kuendelea
kuimarisha usalama huo ili kuepukana na migogoro ambayo hurudisha nyuma
maendeleo.

Mhe. Katambi pia amezipongeza kamati
hizo kwa usimamizi mzuri wa fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo amesema hatua hiyo inachochea
kuongezeka kwa mapato ya ndani katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Aidha ametumia nafasi hiyo kuwaomba
wananchi kuendelea kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan katika shughuli za utekelezaji wa ilani ya CCM ikiwa
lengo ni kuongeza uchumi kwenye jamii na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa
kamati ya ulinzi na usalama Mkoa
wa Shinyanga, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amemshukuru
na kumpongeza Mhe. Katambi kwa uthubutu wake katika kuchochea maendeleo Mkoani
Shinyanga.

Aidha RC Mndeme amemshukuru Rais Dkt.
Samia Suluhu Hassani kwa kuleta fedha zaidi ya Bilioni Mia saba kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo amewahakikishia wananchi kuwa fedha
hizo zitatumika kama ilivyokusudiwa na serikali katika kuleta matokeo chanya
Mkoani Shinyanga.

Amesema serikali ya Mkoa wa Shinyanga
itaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa watu watakao bainika kuvuruga
amani  kwa kufanya uhalifu ikiwemo
vitendo vya ukatili huku akiwataka wakazi wa Mkoa wa Shinyanga kuendelea
kufuata sheria, kanuni na taratibu za Nchi.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa amesema chama hicho kitaendelea kumuunga mkono
Mhe. Katambi katika shughuli zake za maendeleo za kiserikali na chama huku
akimpongeza na kumshukuru kwa zawadi hizo.

Hafla ya kukabidhi zawadi ya nafaka
na vitoeo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi akiwemo Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Gasper Kileo
.

Zoezi la kukabidhi zawadi ya nafaka
na vitoeo vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Naibu waziri
ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas
kwa kamati ya siasa pamoja na kamati ya ulinzi na usalama Wilaya na mkoa wa  Shinyanga likiendelea leo Jumanne Julai 25,2023.

Zoezi la kukabidhi zawadi ya nafaka na vitoeo vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas kwa kamati ya siasa pamoja na kamati ya ulinzi na usalama Wilaya na mkoa wa  Shinyanga likiendelea leo Jumanne Julai 25,2023.

Kilo 200 za mchele pamoja na kuku kumi.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Naibu waziri
ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas wa kwanza upande wa kulia, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa wa pili kutoka upande wa kulia akimpongeza Mhe. Katambi kwa zawadi hizo.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )