MBUNGE MAVUNDE AKABIDHI GARI LA KUSAFIRISHA WAGONJWA KITUO CHA AFYA CHA MKONZE

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde leo amekabidhi gari la wagonjwa(Ambulance) kwa ajili ya kituo cha Afya cha Mkonze Jijini Dodoma.

Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika kituo cha Afya cha Mkonze ambapo gari hili litatoa huduma ya usafirishaji wa wagonjwa wa rufaa kutoka katika kituo hicho ikiwa ni ahadi aliyoitoa Mbunge Mavunde wakati wa kuweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Kituo hicho cha Afya wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018.

“Namshukuru Rais Magufuli kwa ujenzi wa Vituo vya Afya nchini kikiwemo hichi cha Mkonze.Tulikuwa tumebakiza gari tu la wagonjwa na leo tumepata,ni furaha kubwa sana kwamba wananchi wangu sasa watapata fursa ya huduma ya usafirishaji wa wagonjwa tofauti na ilivyokuwa pale awali”

Diwani wa Kata ya Mkonze Mh David Bochela amemshukuru Rais Magufuli kwa ujenzi wa kituo cha Afya cha kisasa ambacho kimerahisisha utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi na pia amemshukuru Mbunge Mavunde kwa ufuatiliaji na upatikanaji wa gari hilo ambalo litasaidia kutatua changamoto ya namna ya kuwasifirisha wagonjwa kutoka kituoni hapo kwenda Hospitali ya Rufaa.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )