MBUNGE MATTEMBE ATOA MSAADA WA KOMPYUTA SHULE YA SEKONDARI ILONGERO

 Mbunge
wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe (wa pili
kushoto) akikabidhi msaada wa kompyuta tano na printa moja zenye thamani
ya Sh.milioni 9.7 katika Shule ya Sekondari ya Ilongero iliyopo Wilaya
ya Singida  mkoani Singida. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya ya Singida,  Eliya Digha, Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi
Paskas Mulagiri,  Diwani wa Kata ya Ilongero,  Issa Mwiru na Mkuu wa
shule hiyo, Ramadhan James.
 Vifaa hivyo vikikabidhiwa. Wengine ni viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo.
Hapa wakionesha ishara ya mshikamano.
Na Dotto Mwaibale, SingidaMBUNGE
wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe ametoa msaada
wa kompyuta tano na printa moja zenye thamani ya Sh.milioni 9.7 katika
Shule ya Sekondari ya Ilongero iliyopo Wilaya ya Singida  mkoani
Singida.Mattembe
akizungumza juzi wakati akitoa msaada huo alisema umelenga kuunga mkono
jitihada za Rais Dkt. John Magufuli za kuhakikisha mpango wa utoaji
elimu bure kwa kila mtoto hapa nchini unaendelea kufanikiwa.
Niliona ni muunge mkono Rais wetu kwa kutoa msaada huu kwa wanafunzi
wetu hawa wa Sekondari ya Ilongero kusoma masomo ya ICT  kwa njia ya
vitendo ili waendane sanjari na ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia.”
alisema Mattembe.Mattembe
alisema dunia hivi sasa imepiga hatua kubwa ya maendeleo hasa katika
matumizi ya teknolojia hivyo wanafunzi wetu wasipojifunza masomo ya ICT
watachelewa kuyafikia mafanikio.
Hivi sasa kila jambo linalofanyika linafanyika kwa njia ya mtandao
ambapo ni lazima muhusika ajue kutumia kompyuta au simu sasa tukiacha
kuwekeza katika masomo hayo itakuwa changamoto kubwa kwa watoto wetu.”
alisema Mattembe.Mkuu
wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Mulagiri ambaye alikuwa mgeni
rasmi katika makabidhiano hayo akizungumza wakati akimkabidhi msaada huo
mkuu wa shule hiyo,  Ramadhan James, alisema msaada huo umekuja wakati
muafaka ambao utawasaidia wanafunzi kujifunza masomo kwa ufasaha hasa
kipindi hiki ambacho dunia inaunganishwa na mitandao.“Pamoja
na yote katika kipindi hiki cha ugonjwa wa Corona kompyuta hizi
zitasaidia wanafunzi wetu kujifunza kwa njia ya mtandao bila ya kuwa
darasani hivyo napenda kumshukuru Mhe.Mattembe kwa kuona mbali na kutoa
msaada huu ambao umefika kwa wakati muafaka”  alisema Mulagiri.Wageni
waalikwa wengine katika  makabidhiano ya kompyuta hizo walikuwa ni 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida,  Eliya Digha, Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Wilaya ya Singida,  William Nyalandu, 
Diwani wa Kata ya Ilongero,  Issa Mwiru,  Diwani Viti Maalumu wa kata
hiyo, Mwanamosha Bakari, Diwani Viti Maalumu, Salma Kundya na Katibu
Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Singida, Naomi David.Wengine walioshuhudia makabidhiano hayo ni walimu wa shule hiyo,wenyeviti wa Serikali za mitaa wa Ilongero  na baadhi ya wazazi.
CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )