MBUNGE AZZA HILAL ATOA MSAADA WA VITI NA NGAO ZA USO ‘FACE SHIELDS’ KUKABILIANA NA COVID 19 KWA WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA

Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa  Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) – Kadama Malunde Ngao za uso ‘Face Masks’ kwa ajili ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga kujikinga na maambukizi ya COVID 19 wanapotekeleza majukumu yao ya uandishi wa habari.

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) ametoa msaada wa Viti kwa ajili ya Ofisi ya Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC) pamoja na Ngao za Uso ‘Face Shield’kwa ajili ya kukabiliana na Maambukizi ya Virusi Vya Corona kwa waandishi wa habari vyote vikiwa na thamani ya shilingi 444,000/=.


Mhe. Azza amekabidhi vifaa hivyo leo Jumatano Mei 6,2020 kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga ,Kadama Malunde katika ofisi hiyo ya waandishi wa habari.


Mhe. Azza amesema Waandishi wa habari ni wadau muhimu katika mapambano ya Virusi vya Corona ndiyo maana ameona ni vyema awachangie vifaa vya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona.


“Sote tunajua tupo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona na tunatambua mchango mkubwa wa waandishi wa habari,mnafanya kazi kubwa katika kuhakikisha kwamba mnaielimisha jamii…Nimewaletea hizi ngao za uso ‘Face Shield’ ili angalau muweze kufunika uso wote..utakuwa umevaa barakoa ndani lakini unafunika uso wako wote ili uweze kufanya kazi zako vizuri”,alieleza Mhe. Azza.

“Kila mwandishi wa habari atapata Ngao ya uso ‘Face Shield’ moja. Ikichafuka unasafisha kwa kitambaa laini kwa maji na sabuni kisha unaendelea kutumia..Ni kitu ambacho siyo cha kutumia na kutupa, unaweza kutumia kwa muda mrefu”,aliongeza Azza.


“Niwasihi tujikinge, tujilinde na tufuate maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya. Hakuna ambalo linashindikana iwapo tutafuata masharti ya wataalamu wa afya”,alisema Azza.

Mbunge huyo pia amekabidhi viti vitano kwa ajili ya ofisi ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga baada ya kuombwa na Mwenyekiti wa SPC kuongeza viti kutokana na idadi kubwa ya waandishi wa habari wanaotumia ofisi hiyo.

“Nitumie fursa hii kumshukuru Mwenyekiti wetu wa Chama cha Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,aliniita siku moja nikaja hapa ofisini,lakini nilipofika tu akaniambia kuhusu upungufu mkubwa wa Viti katika ofisi kutokana na idadi kubwa ya waandishi wa habari…Sikumjibu kitu chochote niliondoka lakini baadaye nikasema niwaletee angalau hivi viti ili kuwaongezea katika ofisi ili muweze kupata sehemu za kufanyia kazi vizuri”,alisema Mhe. Azza.


“Leo nimeleta viti vitano kwa ajili ya ofisi ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga naamini vitawasaidia katika shughuli zenu za uandishi wa habari”,alisema Azza.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa SPC, Kadama Malunde alimshukuru Mbunge huyo wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad kwa msaada wa viti na ngao za uso kwa ajili kujikinga na maambukizi ya COVID 19 kwa waandishi wa habari.


“Mhe. Azza wewe ni mdau mkubwa katika Tasnia ya Habari mkoa wa Shinyanga,tunakushukuru kwa msaada huu wa viti kwa ajili ya ofisi ya waandishi wa habari lakini pia tunakushuru kwa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya COVID 19”,alisema Malunde.

ANGALIA PICHA HAPA

Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimuonesha Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa  Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) – Kadama Malunde Ngao za Uso ‘ Face Shields’ alizoleta kwa ajili ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona pamoja na Viti vitano alivyotoa kwa ajili ya Ofisi ya Waandishi wa  Habari  mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 6,2020. Picha zote na Marco Maduhu,Suleiman Abeid na Frank Mshana

Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimuonesha Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa  Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) – Kadama Malunde Ngao ya uso ‘ Face Shield’ kwa ajili kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa  Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) – Kadama Malunde akivaa Ngao ya uso ‘ Face Shield’ kwa ajili kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona. Ngao hiyo ni sehemu ya ngao 36 zilizotolewa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ili kujikinga na maambukizi ya COVID 19 wanapotekeleza majukumu yao ya uandishi wa habari.

Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa  Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) – Kadama Malunde Ngao za uso ‘Face Masks’ kwa ajili ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga kujikinga na maambukizi ya COVID 19 wanapotekeleza majukumu yao ya uandishi wa habari.
Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa  Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) – Kadama Malunde Ngao za uso ‘Face Masks’ kwa ajili ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga kujikinga na maambukizi ya COVID 19 wanapotekeleza majukumu yao ya uandishi wa habari.
Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa  Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) – Kadama Malunde Viti kwa ajili ya Ofisi ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga.
Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa  Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) – Kadama Malunde Viti kwa ajili ya Ofisi ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza baada ya kutoa msaada wa Viti kwa ajili ya Ofisi ya Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC) pamoja na Ngao za uso ‘Face Shields’ kwa ajili ya kukabiliana na Maambukizi ya Virusi Vya Corona kwa waandishi wa habari.

Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa  Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) – Kadama Malunde ambaye pia ni Mkurugenzi wa Malunde 1 blog akimshukuru Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) kwa msaada wa Viti kwa ajili ya Ofisi ya Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC) pamoja na Ngao za uso ‘Face Shields’ kwa ajili ya kukabiliana na Maambukizi ya Virusi Vya Corona kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga.

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akipiga picha ya kumbukumbu na waandishi wa habari wakiwa wamevaa ngao za uso baada ya kukabidhi msaada wa Viti kwa ajili ya Ofisi ya Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC) pamoja na Ngao za uso ‘Face Shields’ kwa ajili ya kukabiliana na Maambukizi ya Virusi Vya Corona kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga.

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akipiga picha ya kumbukumbu na waandishi wa habari wakiwa wamevaa ngao za uso baada ya kukabidhi msaada wa Viti kwa ajili ya Ofisi ya Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC) pamoja na Ngao za uso ‘Face Shields’ kwa ajili ya kukabiliana na Maambukizi ya Virusi Vya Corona kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga.
Awali Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (kulia) akipokelewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa  Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) – Kadama Malunde alipofika katika ofisi ya SPC leo Jumatano Mei 6,2020 kwa ajili ya  kukabidhi msaada wa Viti kwa ajili ya SPC na ngao za uso ‘Face Shields’ kwa ajili ya kukabiliana na Maambukizi ya Virusi Vya Corona kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga.

Awali Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akinawa mikono kwa maji tiririka na sabuni baada ya kuwasili katika ofisi ya Chama Cha Waandishi wa  Habari Mkoa wa Shinyanga. Aliyevaa nguo nyeusi ni Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa  Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) – Kadama Malunde ambaye pia ni Mkurugenzi wa Malunde 1 blog
Picha zote na Marco Maduhu,Suleiman Abeid na Frank Mshana


CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )