MBUNGE AZZA HILAL AKABIDHI KADI ZA BIMA YA AFYA ALIZOWAKATIA WAZEE KITUO CHA BUSANDA

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad  (CCM) amekabidhi kadi za Bima ya afya iliyoboreshwa (ICHF) alizowakatia wazee 17 waliopo  kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ili wapate huduma za afya bila usumbufu.


Mhe. Azza amekabidhi kadi hizo za bima ya afya leo Ijumaa Mei 8,2020 alizoahidi kuwalipia alipofika katika kituo hicho Oktoba 5,2019 akiwa ameambatana Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kusherehekea Siku ya Wazee Duniani na kutoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula na magodoro. SOMA<<Soma Hapa>>
Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,
Mhe. Azza Hilal Hamad  (CCM) amkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kadi za Bima ya afya iliyoboreshwa (ICHF) alizowakatia wazee 17 wanaolelewa kwenye kituo cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ili wapate huduma za afya bila usumbufu. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiangalia kadi za bima ya afya kwa ajili ya wazee 17 waliopo katika kituo cha Busanda.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikabidhi bima za afya kwa wawakilishi wa wazee waliopo katika kituo cha Busanda zilizotolewa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad  (CCM).

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikabidhi bima za afya kwa wawakilishi wa wazee waliopo katika kituo cha Busanda zilizotolewa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad  (CCM).

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikabidhi Paroko wa Parokia ya Busanda,Padri Josephat Mahalubima za afya 17 zilizotolewa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad  (CCM) ili akawakabidhi wazee waliopo katika kituo cha Busanda.
Picha zote na Kadama Malunde 

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )