MBUNGE ASIA HALAMGA KULETA NEEMA SHULE YA SEKONDARI YA NANGWA

 

Mbunge wa Viti Maalum Mhe: Asia Halamga ameaahidi kuwatafutia Vitabu pamoja na Walimu wa masomo ya Sayansi katika Shule ya Sekondari ya Nangwa Wilayani Hanang Mkoani Mayara mara baada ya kupokea taarifa kuwa Wanafunzi wengi wanaomaliza Shule bila kutumia vitabu vya mitaala mbalimbali ili kukuz Elimu.

Akizungumza mara baada ya kusikiliza changamoto hizo Mbunge Asia Halamga amesema yeye pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo la Hanang katika kutatua changamoto hizi “Changamoto zenu nimezipokea naahidi kushirikiana na ninyi sambamba na Mbunge wenu wa Jimbo kuzitatua ili muweze kufundisha katika mazingira na watoto wa wapiga kura wetu waweze kupata elimu bora na itakayowawezesha kufanya vizuri na kukuza kiwango cha elimu ktika Wilaya hii ya Hanang”

Mhe. Asia ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Hanang kwa kutoa kfedha kutoka mapato ya ndani kwa ajili ya ujenzi wa madarasa . Aidha amewapongeza wananchi wa kata husika kwa kuchangia ujenzi huo ili kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli,

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )