MBEYA CITY V SIMBA NGOMA NZITO LEO SOKOINE


UONGOZI wa Simba umesema kuwa leo utapambana kupata pointi tatu kwenye mchezo wao utakaopigwa majira ya saa 10:00 jioni Uwanja wa Sokoine.

Akizungumza na Saleh Jembe,  Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa leo ili kufikia malengo yao ya kutwaa ubingwa.

“Utakuwa mchezo mgumu hilo lipo wazi lakini kikubwa ambacho tunahitaji ni pointi tatu muhimu. 

“Wapinzani wetu Mbeya City wanapambana kushuka daraja Daraja wanapambana kupata pointi tatu hivyo mashabiki watupe sapoti,”.

 Simba ipo nafasi ya Kwanza ikiwa na pointi 75 baada ya kucheza mechi 30 huku Mbeya City ikiwa na pointi 30 baada ya kucheza mechi 30 ikiwa nafasi ya 18.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )