Mbaroni kwa tuhuma za mauaji ya mzee kisa kuku.

Jeshi la polisi mkoani Mtwara linamshikilia
Mukhsin Selemani mwenye umri wa miaka 24 mkazi wa kijiji cha Libobe wilaya ya
Mtwara, kwa tuhuma za kumuua Hassan Mtipa kwa panga katika tukio la wizi.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa
Mtwara, – Mark Njera amesema tukio hilo limetokea katika kijiji cha Mayanga,
ambapo Mukhsin aliingia kwenye nyumba ya Mtipa mwenye umri wa miaka 67 kwa
lengo la kuiba kuku, sola na nguo.

Baada ya kukamatwa na polisi, mtuhumiwa huyo
amekiri kuiba vitu hivyo pamoja na kufanya mauaji hayo.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )