Mavunde agawa vifaa mbalimbali vya kujikinga na ugonjwa wa corona kwa Shule zote.

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde  amegawa vifaa mbalimbali vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa COVID 19
kwa Shule zote za Sekondari za umma na binafsi zenye kidato cha Sita.

Mavunde amekabidhi  vifaa hivyo vyenye
thamani ya zaidi ya Tsh 2,000,000 kwa wakuu wa Shule za Sekondari katika eneo
la Jiji ya Dodoma ikiwa ni siku ya kwanza kwa wanafunzi wa kidato cha sita
kurejea tena shuleni baada ya agizo la Mh Rais Dr John Pombe Magufuli kuhusu
kufunguliwa tena kwa Vyuo na Shule.


“Baada ya Shule kufunguliwa tena nimeona
kama Mbunge niunge mkono agizo la Mh Rais kwa kuhakikisha kwamba wanafunzi
katika Jimbo langu wanasoma katika mazingira salama na ndio maana nimetoa
majaba yenye uwezo wa kuhifadhi lita 1760,Sabuni lita 500,ndoo 50,sabuni boksi
25,Vitakasa mikono 500 na ndoo 50.

Rai yangu ni kuwataka wanafunzi wote wa kidato
cha Sita kutumia muda huu kikamilifu kwa kusoma kwa bidii ili kufanya vizuri
katika mitihani yenu ya mwisho ili kuendelea kulipaisha Jiji la Dodoma kwenye
sekta ya Elimu”Alisema Mavunde

Akishukuru kwa niaba ya Wakuu wa Shule wa
Sekondari,Mwl. Aloe Lyimo amemshukuru Mbunge Mavunde kwa msaada mkubwa uliokuja
kwa wakati muafaka na kuahidi kutumia vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )