MASHINDANO YA RIADHA YA WATOTO (AYAC) KUFANYIKA MARCH 28 MWAKA HUU ARUSH

 

 

Ferdinand Shayo ,Arusha.

 

Mashindano ya riadha ya Arusha Youth Athletic Championship  yanatarajia kufanyika March 28 mwaka huu katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid huku yakilenga  kuibua vipaji vya watoto  katika mchezo wa riadha .

 

Mratibu wa mashindano ya Arusha Youth Athletic Championship (AYAC)  Juliana Msuva amesema kuwa watoto kutoka shule 40 wanatarajia kushiriki mbio hizo za aina yake  zinalenga kuibua,kukuza na kuendeleza vipaji vya riadha.

 

Juliana anasema kuwa Zaidi ya watoto 300 watashiriki mbio hizo kuanzia umri wa miaka 6 mpaka 21 .

 

Kwa upande wake Makamu Raisi wa Chama Cha Riadha Tanzania (Rt) Filbert Bayi amepongeza waandaaji wa mashindano hayo kwa kujenga misingi bora ya mchezo wa riadha suala litakalosaidia kupata wanariadha bora watakaoliwakilisha taifa katika michezo ya kimataifa.

Afisa michezo jiji la arusha Benson Maneno amesema kuwa serikali itaendelea kuunga mkono mbio hizo ili ziweze kufanikiwa na kuleta matokeo chanya katika mchezo wa riadha.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )