MAONESHO YA NNE MFUKO WA PROGRAM ZA UWEKEZAJI WANANCHI KUFUNGULIWA NA KASSIM MAJALIWA.

 

Arusha

Waziri Mkuu wa jamuhuri wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa  anatarajiwa kufungua maonesho ya nne ya mfuko wa programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi mnamo februari 9, 2021 yanayofanyika kitaifa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoa Arusha.

Akiongea na waandishi wa habari kaimu mkurugenzi wa uwezeshaji na ushiriki wa watanzania katika uwekezaji kutoka baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) Esther  Mbaga ambao ndio waandaji wa maonesho hayo yaliyoanza leo Februari 7 hadi 13 mwaka huu huku.

Esther Mbaga  alisema kuwa baraza hilo limeratibu maonesho hayo ili kuwawezesha wananchi kufahamu mifuko na programu mbalimbali za uwezeshaji wananchi zilizopo hapa nchini kwa lengo la kuhakikisha kuwa wanafahamu fursa zinazopatikana na kujua taratibu za kuweza kunufaika mifuko hiyo.

“Katika maonesho haya  kuna takribani mifuko na programu za uwezeshaji 25 , taasisi mbalimbali za serikali na sekta binafsi ambazo zinafanya shughuli za kuwezesha wananchi kiuchumi 77 pamoja na wajasiriamali 200 kutoka katika halmashauri mbalimbali  na kutoka katika mikoa ya kanda ya kaskazini ambao nao wamekuja kuonyesha bidhaa zao,”Alisema.

Alifafanua  kuwa katika maonesho ya mwaka huu wana kauli mbiu isemayo “Mifuko na programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa maendeleo ya taifa” kwasababu wanajua mifuko na programu za uwezeshaji zina jukumu kubwa katika kuwawezesha watanzania ili kuweza kushiriki kikamilifu uchumi wa nchi.

Alieleza maonesho hayo yatawawezesha wananchi wa kawaida kwasababu kuna mifuko mbalimbali inayowezesha wananchi kwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu na inayotoa ruzuku ikiwa mingine inatoa dhamana hivyo wananchi wa Arusha, kanda yote ya kaskazini na sehemu nyingine watembelee maonesho hayo ili kuweza kushiriki lakini kunufaika.

Hata hiyo maonesho hayo yaliyoanza Februari 7 na kufunguliwa rasmi Februari 9 yanatarajiwa kuhitimishwa Februari 13 na waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera bunge kazi ajira vijana na watu wenye ulemavu Mhe Jenista mhagama.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )