MAOFISA WANNE WA NEMC KIZIMBANI WAKIKABILIWA NA KESI YA UHUJUMU UCHUMI

Maofisa
wanne wa Baraza la usimamizi wa Mazungira (NEMC) wakiwa katika Mahakama
ya Hakimu mkazi Kisutu  jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na kesi ya
uhujumu uchumi.

Na Karama Kenyunko 


MAOFISA
wanne wa Baraza la usimamizi wa Mazungira (NEMC) wamefikishwa katika
Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi
yenye mashtaka tisa yakiwemo ya kughushi, kula njama, utakatishaji fedha
na kuisababishia Mamlaka hasara ya Sh. Milioni 18.5..
Katika
hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa Serikali
Janeth Magoha akisaidiana na Stanley Lugola na Sofia Nyanda mbele ya
Hakimu mkazi Mkuu Huruma Shaidi imewataja washtakiwa hao kuwa ni, 
Deusdedith Katwale, Magori Matiku, Obadia Machupa ma Lydia Nyinondi
ambae ni Mhasibu msaidizi wa Nemc
Katika
shtaka la kwanza washtakiwa wote wanadaiwa kati ya Juni Mosi 2016 na
Julai 30, 2017 ndani ya jiji la Dar es Salaam na Dodoma, walikula njama
ya kutenda makosa ya kughushi, kutoa nyaraka iliyogushiwa, kuisababishia
mamlaka hasara na kutakatisha fedha.
Katika
mashtaka ya kughushi imedaiwa kati ya Agosti Mosi 2016 na Septemba 6,
2017 huko Kinondoni ndani ya jiji Dar es Salaam na Mkoani Dodoma
Mshtakiwa Katwale  alighushi ripoti ya kutathmini mazingira ya mradi wa 
Kituo cha Mafuta cha Ibra General Enterprises lililopo kitabu namba 132
Block T Chadulu Area A Dodoma Kwa dhumuni la kuonesha kwamba tathmini
ya mazingira juu ya mradi huo ilikuwa imefanyika huku akijua kuwa siyo
kweli.
Pia
mshtakiwa huyo anadaiwa kughushi kikao cha tathmini ambayo ni nyaraka ya
‘Minutes for Technical Advisory Committee (TAC’ kuonesha kwamba kikao
hicho kilichofanyika huki mshtakiwa Lydia akidaiwa kuwa Julai 5, 2016
maeneo ya Ofisi za NEMC Kinondoni, alighushi risiti yenye thamani ya Sh
milioni 18.5 kuonesha kuwa zimelipwa kwa NEMC.
Katika
shtaka la tano, imedaiwa kuwa, kati ya Juni Mosi, 2016 na Julai 30,2017
katika Ofisi za NEMC Kinondoni, mshtakiwa Katwale aliwasilisha nyaraka
ya uongo kwa Mkurugenzi wa NEMC kuhusu mradi wa mafuta wa Ibra General
Enterprises kuonesha kuwa ukaguzi wa mradi huo  ulifanyika huku akijua
kuwa siyo kweli.
Aidha, mwendesha Mashtaka Luoga, alidai Julai 5,2016, Matiku aliwasilisha nyaraka ya uongo ya risiti kwa Yunis Mfala.
Imeendelea
kudaiwa kuwa, washitakiwa hao pia wakiwa watumishi wa NEMC walikiuka
kifungu cha 29 cha Sheria ya Usimamizi Mazingira iliyofanyiwa
marekebisho mwaka 2002 na hivyo, kujipatia Sh milioni 18.5 kwa ajili
yao.
Katika
mashitaka ya kusababisha hasara, imedaiwa kati ya Juni Mosi, 2016 na
Julai 30 2017 huko Kinondoni, washtakiwa hao kwa pamoja wakiwa
watumishi  wa Nemc wakiwa na nia ovu walisababisha Mamlaka hiyo hasara
ya Sh milioni 18.5.
Katika
shtaka la tisa la utakatishaji imedaiwa, Sikh nanmahali hapo washtakiwa
hao walijipatia kiasi hicho cha fedha toka kwa Mfala ambaye ni mmiliki
wa mradi wa kituo cha mafuta cha Ibra General Enterprises huku wakijua
kuwa fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la kughushi.
Washitakiwa
wamekana mashtaka nankwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika
kesi hiyo umekamilika na kwamba Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP)
ametoa kibali cha kusikiliza kesi hiyo.
Wakili
wa utetezi, Rugemeleza Nshala alidai wanaomba dhamana kwa wateja wao
kwa sababu Mahakama Kuu imeshatoa uamuzi kwamba mashitaka ya
utakatishaji fedha yanadhaminika.
Hata
hivyo upande wa mashtaka waliongoza na wakili Luoga ulipinga vikali hoja
hiyo na kusema kuwa mashtaka ya utakatishaji fedha hayafahamiki na
kwamba wanafahamu uwepo wa kesi ya kikatiba ambayo iliamuriwa na
Mahakama Kuu na kuongeza kuwa, mahakama iliwapa muda wa miezi 18
serikali kufanya mabadiliko ya sheria iliyozuia dhamana kwa Washtakiwa
wa makosa ya utakatishaji fedha kwamba yadhaminike na kabla ya hapo
sheria iendelee kutumika kama kawaida.
Hata hivyo, Nshala alidai mahakama inayo mamlaka ya kutoa amri yoyote kuhusu dhamana ambayo ni haki ya kikatiba ya washitakiwa. 
Akitoa
uamuzi, Hakimu Shaidi alisema licha ya Mahakama Kuu kutoa uamuzi wa
mashitaka hayo kudhaminiwa lakini pia imetoa masharti kwamba  jamhuri
irekebishe sheria hiyo kwa miezi 18 hivyo maombi hayo ya dhamana kwa
sasa si sahihi na kama mtu ataona si uamuzi sahihi aende Mahakama Kuu
kwa ajili ya kufanya mapitio.
Amesema,
mahakama ya kisutu imefungwa mikono haiwezi kutoa dhamana hivyo,
washitakiwa wataendelea kubaki rumande  hadi Juni 18, mwaka huu kwa
ajili ya kusomewa maelezo ya awali.
CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )