MANISPAA YA ILALA YAANZA OPARESHENI KUKAGUA MAPATO

Mfanyabishara wa Jumla Buguruni Venas Mushi  ,akiongea na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri (katikati) wakati wa oparesheni ya kukagua mapato wengine ni maafisa wa Ilala (PICHA NA HERI SHAABAN)
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala(katikati) Jumanne Shauri akikagua leseni katika oparesheni ya kukusanya mapato inayoendelea (PICHA NA HERI SHAABAN)
…………………….

NA HERI SHAABAN

MANISPAA ya Ilala imeanza oparesheni endelevu ya ukaguzi wa Mapato katika maduka ya wafanyabiara.

Oparesheni hiyo imeongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala  Jumanne Shauri na Maafisa wa Mapato  .

Dhumuni la ziara hiyo kukusanya   kodi  kuwafuata wafanyabiashara ambao hawajalipa kodi.

“Kuanzia leo vituo vya kukusanya mapato vipo wazi Jumamosi,Jumapili na siku za Sikukuu
vilivyopo Buguruni, kata, Ukonga Kata na katika jengo la Arnatogluo “alisema Shauri.

Mkurugenzi Shauri amewataka Wafanyabiashara kutii sheria bila shuruti kwani msako kwa wasiolipa leseni, tayari umeanza katika halmashauri hiyo.

Mtu ambaye atakutwa ajalipa leseni kwa muda ulipangwa atatozwa faini  hivyo kwepa usumbufu lipa katika vituo vya halmashauri serikali iweze kupata mapato yake ufanye biashara zako bila kusumbuliwa.

Aliwataka wananchi kulipa leseni kwa wakati kuogopa usumbuliwa ada ya leseni ya biashara inatozwa kwa mujibu wa sheria ya leseni za biashara ya mwaka 1972 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2014 ,kwa wafanyabiashara wasio na leseni maombi ufanyika mahala popote na wakati wowote.

Kwa upande wake mfanyabiashara wa duka la jumla Buguruni Venance Mushi amelalamikia Serikali akitaka iwachukulihatua Madali wanawalibia biashara zao kwa kitendo cha kukamata wateja  wakati wateja wanayajua maduka ya kunuua bidhaa kwa bei ya jumla na rejaleja.

Mushi alisema kwa sasa biashara sio nzuri  Madalali pia wamechangia  katika kuwakamata wateja hivyo ameomba serikali kulichukulia hatua.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )