MAKAMU MWENYEKITI UVCCM TAIFA , BI TABIA MAULID MWITA (MNEC) AFANYA ZIARA MKOA WA MBEYA

Makamu Mwenyekiti UVCCM Taifa Bi Tabia Maulid Mwita (MNEC) amefanya Ziara Mkoa wa Mbeya na kupokelewa na Viongozi wa Chama na Serikali wakiongozwa na Mwenyeji wake Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Ndg.Mohamed Mashango  pamoja na wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji Mkoa.

Makamu amekagua ujenzi wa Nyumba za Makatibu UVCCM Mkoa na Wilaya Mbeya jiji na kufurahishwa na ujenzi huo huku akiwataka viongozi wa Jumuiya waende kasi na ujenzi huo.

Makamu pia alipata nafasi ya kuwa mgeni rasmi  kwenye kongamano  la kikundi cha kimkakati kijulikanacho kama “ MABINTI CCM  ambacho nacho ni zao la UVCCM Mkoa wa Mbeya.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )