MADEREVA 13 WAMESIMAMISHIWA LESENI ZAO KWA MUDA WA MIEZI SITA.

 Kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Tanzania SACP Fotunatus Musilimu akiwa na dereva aliyekuwa anaendesha basi bila kufuata utaratibu na sheria za barabarani.

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Madereva 13 wamesimamishiwa
leseni zao kwa muda wa miezi sita na kutokujihusisha na kazi ya udereva wa
magari makubwa kwa kosa la kuvunja sheria za uslama barabarani kwa kuendesha
magari hayo kwa mwendo kasi.

Kamishina msaidizi mwandamizi
wa polisi Tanzania SACP Fotunatus Musilimu ameeleza kuwa suala la ajari hapa
nchini halitakiwa hata mara moja hivyo dereva yoyote atakayekiuka sheria za
usalama barabarani ni lazima atachukuliwa hatua za kisheria.

Ameeleza kuwa madereva hao wote
waliochukuliwa leseni zao hawaruhusiwi kujishugulisha na kzi yoyote ya udereva
wa mabasi makubwa ndani ya miezi sita ila wanachoruhusiwa ni kufanya kazi za
udereva katika magari madogo.

Kamishina huyo ameeleza kuwa
lengo la kufungiwa kwa leseni hizo ni kudhibiti mwendokasi , kupunguza na
kumaliza kabisa ajari barabarani ili kuokoa maisha ya watanzania.

Aidha ameeleza kuwa kumekuwa na
desturi ya baadhi ya madereva na wapiga debe kubashiri kwa dereva atakayewahi
kufika mapema zaidi na kumpatia kiasi cha fedha kama sehemu ya pongezi na
hamasa kwa madereva wengine kuendesha magari kwa mwendo kasi jambo ambalo ni
hatari kwa usalama.

Wakizungumza baadhi ya
makondakta na madereva wamekiri kuwepo kwa tabia ya kubert kwa baadhi ya
madereva na makondakta na kulaani kitendo hicho kwani kinahatarisha usalama wa
abiria na nikinyume na sheria za usalama barabarani.
CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )