Ligi ya Kikapu Tanga kurindima hivi karibuni.

 

NA DENIS CHAMBI, TANGA.

NANI
atakwenda kunyakua taji la ligi ya mpira wa kikapu mkoa wa Tanga msimu
huu?  Pengine hili ni swali ambalo wanafamilia wa mchezo huo wanajiuliza
ambapo utepe wa michauano hiyo utakwenda kukatwa July 29 huku viwanja
vya Korogwe na Mkwakwani Tanga vikitumika kwa michauano hiyo.

Michauano 
hiyo  ambayo mwaka huu itajulikana kwa jina  ‘TRBA’  Mkonge City Basket
ball ligi  itahusisha timu 6 za wanaume zitakazoingia katika
kinyang’anyiro  hicho ambazo ni Tanga United, Deep sea ( Harbours 
Club),
Ng’e, Korogwe Heat, Bandari Tanga pamoja na  Ngamiani  Kings.
Akizungumza
katibu wa chama cha mpira wa Basketball mkoa wa Tanga Riziki Mgude
amesema kuwa maamuzi waliyofanya kucheza ligi hiyo katika viwanja viwili
vya wilaya tofauti ni mpango wao wa kuzidi kuongeza  hamasa na wigo
mpana wa mchezo huo katika wilaya zote zilizopo sambamba na kuipa
Korogwe Heats thamani kuipunguzia safari za kwenda na kurudi kwaajili ya
kuweza kushiriki.
“Ligi
ya mpira wa Kikapu mwaka huu itajulikana kama TRBA Mkonge City
Basketball ligi  inatarajiwa kuanza July 29 ambapo wikiendi hii ya
tarehe 23 tutakutana kwaajili ya mechi ya ufunguzi na mwaka huu tuna
timu 6 mwaka jana tulikuwa na timu 4 na viwanja vitakavyoyumika vitakuwa
ni viwili vya Mkwakwani na Korogwe , tutacheza mizunguzo miwili halafu
wale wawili wa juu watakwenda kucheza fainali” alisema Mgude.
Katibu
huyo amesema kuwa kuna maboresho makubwa wameyafanya katika upande wa
zawadi kwa washindi wa michauano hiyo msimu huu ukitofautisha na ule wa
mwaka 2022 hii ikilenga hasa kuongeza chachu ya ushindani kwa timu zote
zitakazochuana kumtafuta bingwa wa 2023.

Ni matumaini yetu kwamba zawadi zitakuwa lukuki mwaka jana tulitoa
vikombe viwili kwa kila mshindi na medal kwa mshindi wa kwanza na wa
pili mwaka huu tunataka tuongeze zawadi nyingine ili ligi ipate thamani
na kila timu itayoa kiingilio cha shilingi laki mbili  na bado tupo
kwenye mchakato wa kutafuta wadhamini ili kutuongezea thamani ligi yetu”
aliongeza Mgude.
 

Mabingwa watetezi wa kombe la ligi ya Mpira wa kikapu mkoa wa Tanga Bandari Tanga  kwa mwaka 2022

Kikosi cha timu ya Korogwe heats  kitakachoshiriki ‘TRBA’  Mkonge City Basket
ball ligi mwaka huu 2023.

Kikosi cha timu ya Habours Club(Deep see) kitakachoshiriki ‘TRBA’  Mkonge City Basket
ball ligi mwaka huu 2023.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )