Kinana amuomba radhi Rais Magufuli.

Baada ya kimya cha muda mrefu hatimaye katibu mkuu mstaafu wa chama
cha mapinduzi Comrade Abdulrahaman Kinana amejitokeza hadharani na
kumuomba radhi mwenyekiti wa chama cha mapinduzi taifa dakta John Pombe
Magufuli kwa matukio mbalimbali yaliyojitokeza baada ya kung’atuka
katika uongozi chama hicho.

Kinana pia amewaomba radhi watanzania na wanachama wa CCM aliowakwaza kwa kitendo kilichotokea.

Kinana akiwa na baadhi ya viongozi wakongwe wa chama hicho walipewa
adhabu hiyo baada ya mazungumzo yao ya simu kunaswa wakimteta rais wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania dakta John Pombe Magufuli na kusambaa
katika mitandao mbalimbali ya kijamii hali iliyosababisha uongozi wa CCM
kuwaita na kuwahoji, viongozi hao wakiwemo wastaafu na waliopo
madarakani.

Awali akizungumzia adhabu aliyopewa na chama Kinana amekiri kutokea
kwa jambo hilo na kudai kuwa kama binadamu alighafilika na kudai kuwa
akiwa ni mkongwe katika chama hicho adhabu ni utaratibu uliopo katika
chama chochote kwa kiongozi au mwanachama anapokosea.

Wakati huo huo Komrade Kinana ametembea ofisi za CCM mkoa wa Arusha
na kuzungumza na mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Arusha Zelothe
stephen zelothe.

Tangu sakata hilo litokee Katibu mkuu huyo mstaafu wa CCM
Abdulrahamani Kinana hakuwahi kusikika katika vyombo vya habari wala
mitandao ya kijamii kuzungumzia sakata hilo.

HT: Channel Ten

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )