Kaya 229 zapatiwa msaada wa Chakula Mkinga.

  

NA DENIS CHAMBI, TANGA. 
JUMLA ya Kaya 229 kutoka Vijiji mbalimbali wilayani
Mkinga Mkoani Tanga zimepatiwa Msaada wa Chakula kupitia Shirika la
World Vision ikiwa ni sehemu ya Kukabiliana na Uhaba wa Chakula kwenye
baadhi ya maeneo yaliyokumbwa na ukame kwa miaka miwili mfululizo. 

Baadhi
ya wananchi wilayani humo wamekuwa wakikabiliwa  na  tatizo la Uhaba wa
Chakula kwa kipindi cha Miaka miwili mfululizo hali inayopelekea kupata
Lishe ndogo kutokana na watoto wao kula Mlo mmoja Kwa siku badala ya
milo mitatu
Wakizungumza
mara baada ya kukabidhiwa msaada huo wa Chakula Wananchi wa Vijiji zaidi
ya 8 wikayani humo wamesema wamekuwa wakikabiliwa  na Uhaba wa Chakula
kwa kipindi cha Miaka miwili sasa jambo linalopelekea afya zao kudumaa
na hatimaye watoto kushindwa kufanya vizuri pindi wawapo mashuleni. 
“Watoto
wetu wanatakiwa wale kutwa mara tatu lakini wakwetu kutwa wanakula mara
moja tuu hii ni changamoto kubwa sana inayotukabili sisi wazazi
tunanyongeka sanaa, “alisema mmoja wa wananchi hao. 
Baadhi
ya wananchi wengine wamesema wanasumbuliwa na Upatikanaji wa Pembejeo
za Kilimo katika Vijiji vyao ambapo wameliomba Shirika la World Vision
kuwawezesha Vikundi vya Ulemavu ili waweze pia kupatiwa Msaada wa
Pembejeo
“Tuishukuru
World Vision kwa hiki walichotuletea leo tunaomba watutembelee pindi
wanapokwenda kwenye miradi yao sisi walemavu tuna vikundi vyetu vya
walemavu waje wavione waone nini kinatukwamisha hususani kwenye pembejeo
za kilimo maana walemavu sisi hatuoni wengine wamekatwa miguu lakini
watoto tulionao ndio wanatusaidia, “alisema Mmoja wa walemavu hao. 
Kwa
Upande wake Afisa Mtendaji wa Kijiji Cha Maforoni wilayani Mkinga
Albertina Makungu amesema Katika mwaka wa 2021 na mwaka 2022 walipatwa
na Changamoto ya Ukame katika maeneo ya wilaya ya Mkinga, ambapo
amelishukuru Shirika hilo kwa kutoa Msaada kwa watu wenye Uhitataji wa
Chakula
“Kweli tuna janga
la njaa tunakula kwa shida tunashukuru zaidi kwa msaada huu tumekuwa na
janga la njaa kwa muda mrefu sasa kaya hizi na familia hizi zimepata
shida ya chakula kwa miaka miwili mfululizo, “alisema Makungu. 
Meneja
wa Mradi wa World Vision katika Wilaya ya Mkinga Evodia Chija amesema
Shirika hilo kupitia Viongozi wao limeamua kuwagusa waathirika wa Janga
la Njaa kutokana na ukame katika baadhi ya maeneo, ambapo wameweza
kuwachangia Maharage na mahindi kilo 2000
Amesema
lengo la kutoa msaada kwa makundi ya wenye Ulemavu na watoto ambao
wanaishi katika mazingira magumu ni ili na wao waishi kwa furaha kwa
kupata tumaini kwenye maeneo yao kama watu wengine.
“Wafanyakazi
wa World vision kwa ushirikiano wao na upendo wao tuliweza kukusanya
kiasi cha shilingi milioni 7.5 ambazo kwa furaha kubwa viongozi wetu
wakazielekeza zile fedha zilizopatikana zije kusaidia watoto wenye
uhitaji katika eneo la mradi wa Mkinga, “alisisitiza Chija. 
“Tumetoa
msaada wa Maharage,  unga kilo 2000 wenye virutubishi kwenye kaya hizi
lakini kati ya kaya hizo Kaya 30 ni za watu wenye ulemavu,  watoto ambao
ni wasajiliwa kwenye miradi ya World Vision wako kaya 136,”alibainisha
Chija. 
Meneja
wa Mradi wa World Vision katika Wilaya ya Mkinga Evodia Chija akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoa msaada huo.

Badhi ya kaya zilizonufaika na msaada wa chakula kutoka World Vision

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )