KATIBU WA CCM MWANZA AKISHIRIKI SHUGHULI ZA UJENZI


Salum
Kalli ambaye ni Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akishiriki kuweka
tyries kwenye maegesho ya magari ya jengo la ofisi za CCM Mkoa
jana.Mradi huo wa eneo la maegesho unakarabtiwa na kulifanya la kitega
uchumi.

Katibu
wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli (mwenye shati la kijani),
akishirikiana na wasimamizi wa mradi ya ukarabati wa maegesho ya magari
kwenye ofisi za CCM mkoa jana.

Picha na Baltazar Mashaka

********************************
NA BALTAZAR MASHAKA, Mwanza

UBORESHAJI wa ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza unazidi kupamba moto na unazifanya madhari zake kuvutia.

Kauli
hiyo ilitolewa juzi na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli
wakati akihojiwa na Uhuru kuhusu uboreshaji huo wa ofisi miradi mingine
ya maendeleo.


Alisema uboreshaji wa ofisi ya CCM Mkoa wa Mwanza
unaofanywa chini unazidi kupamba moto na kufanya madhari yake kuvutia na
kuirejesha katika ubora wake.


Alisema wamefanya maboresho ya
kupaka rangi jengo lote la ofisi hiyo ya CCM mkoa (ndani na nje) pamoja
na kuliwekea malumalu (vigae) kwenye sakafu baada ya miaka mingi kupita
na hivyo kufanya madhari yake yavutie.


“Kamati ya Siasa ya Mkoa
chini ya Mwenyekiti Dk. Anthony Diallo uliamua kufanya maboresho ya
Uwanja wa CCM Kirumba uliotumika kwa maadhimisho ya Sherehe za Miaka 58
ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri, tuliboresha Jukwaa Kuu na kujenga
majukwaa mengine madogo mawili kwenye uwanja huo,”


“Maboresho
mengine yaliyofanyika ni ukarabati mkubwa wa jengo la ofisi yaa CCM Mkoa
ambao ulikuwa ni kulipaka rangi ndani na nje pamoja na kuliwekea vigae
kwenye sakafu.Yote hayo yamefanyika kwa ajili ya maendeleo na
kusababisha vikao vya maandalizi ya ilani vya Kamati Kuu na Halmashauri
Kuu ya Chama vilifanyika hapo,”alisema Kalli.


Alisema kazi kubwa
iliongezeka ni ya ukarabati wa eneo la maegesho ya magari ambalo
liliharibika ambapo kazi inayofanyika ni kuliwekea tyries baada ya
kukamilika litatumika kiuchumi
CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )