JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA NCHINI WAISHUKURU SERIKALI

NA DENIS CHAMBI, TANGA.

JUMUIYA ya Wafanyabishara nchini july 26 imekutana na Wafanyabishara
wa Mkoa wa Tanga kwaajili ya kusikiliza kero pamoja  na kuchukua maoni mbalimbali kwaajili ya
kuyapeleka Serikalini ikiwa ni agizo la waziri mkuu Kassimu Majaliwa alilolitoa
hivi karibuni alivyofanya mkutano na Jumuiya ya Wafanyabishara nchini na kuunda
kamati maalumu itakayokusanya maoni kila Mkoa ili kuweza kuyafanyia kazi ikiwa
ni lengo la Serikali kuweka mazingira rafiki katika sekta ya Uchumi.

Akizungumza mara baada ya mkutano huo mwenyekiti wa jumuiya
ya Wafanyabishara nchini Hamis Livembe amesema kuwa pamoja na kuzunguka kila Mkoa
kwaajili ya kukusanya maoni hayo wana lengo pia la kusajili wanachama wapya
katika jumuiya hiyo huku akiipongeza Serikali kuwa kukubali kuwasikiliza
wafanyabishara kutokana na kero mbalimbali zinazowakabili na hatimaye kuzipatia
ufumbuzi .

“Tumekuwa na ziara za kawaida kuzunguka kila mkoa kwaajili
ya kusikiliza kero changamoto na mafanikio yao kutoka kwa wafanyabishara ,
lakini pia kusajili wanachama wapya na pale wanapokosoa wanakosoa na pale
wanapopongeza wanapongeza yale maoni yote huwa tunayachukuwa”.

“Sasa hivi wafanyabishara wana hamu kubwa baada ya lile
sakata kubwa la kufungwa maduka kule Kariakoo Dar es salaam imeundwa kamati
baada ya kurudi huko wanataka watusikie  kuna nini kipya lakini pia tunatoa mrejesho
kwa yale ambayo tayari tumeshapata majibu na viko vingine vichache katika
mchakato kwahiyo tunaendelea na ziara ya kuyakusanya maoni ya wafanyabiashara”
alisema Livembe

“Tunaweka shukrani zetu kwa serikali kupitia majukwaa yetu
ya wafanyabishara kutokana na jinsi walivyotupokea lakini pia  walivyofungua milango kwa njia ya mazungumzo
na wafanyabishara kwaajili ya kupata muafaka namna walivyotupokea  kukaa mezani tujadiliane kwa namna gani
bishara zetu ziendeshwe”aliongeza

Kwa upande wake katibu wa Jumuia ya Wafanyabishara wa Mkoa
wa Tanga Masoud Ismaili licha ya kuishukuru serikali amesema kuwa  bado zipo changamoto lukuki zinazo wakabiri Wafanyabishara
ikiwemo kupandishiwa makadirio ya kodi sambamba na usumbufu wa ushuru kutoka
katika taasisi mbalimbali mambo ambayo yanawakatisha tamaa hata ya ulipaji kodi
kwa hiari.

 “Watu wanalalamika
wamepigwa makadirio makubwa ya ulipaji kodi nashauri muwatoze watu fedha kidogo
ili walipe kodi kwa wakati na sio kukaa kwenye na takwimu ofisini ambazo hazina
uhalisia wa Biashara husika ninazo barua za watu mbalimbali wanatozwa kodi
kubwa, malalamiko yapo nafikiri wahusika wameyasikia nilikuwa naomba
yachukuliwe hatua, Wafanyabishara wote wanataka walipe kodi na sio kukwepa
kulipa kodi “  alisema Masoud

 

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )