JPM AMWAGA KIWANDA KIKUBWA CHA KUKU NA KLINIKI YA KISASA YA MIFUGO SINGIDA

Waziri
wa Mifugo na Uvuvi (mwenye kofia nyeusi) Luhaga Mpina akishiriki
katika zoezi la ujanjaji wa mifugo kitaifa pamoja na wataalam wa mifugo
lililofanyika leo kwenye kijiji cha Kinyangiri wilayani Mkalama mkoani
Singida ambapo Serikali imeahidi kuwezesha kujenga kiwanda kikubwa cha
machinjio ya kisasa kitakacholisha Tanzania na nchi mbalimbali duniani.

Waziri
wa Mifugo na Uvuvi (mwenye kofia nyeusi) Luhaga Mpina wa kwanza kulia
akifuatiwa na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida ambaye pia ni Mkuu
wa Wilaya ya Mkalama Injinia Jackson Masaka na Mwakilishi wa Katibu
Tawala wa Mkoa wa Singida ndugu Beatus Choaji wakiwa kwenye sherehe za
uzinduzi wa ujanjaji wa mifugo kitaifa pamoja na wataalam wa mifugo
lililofanyika leo kwenye kijiji cha Kinyangiri wilayani Mkalama mkoani
Singida.

Waziri
wa Mifugo na Uvuvi (mwenye kofia nyeusi) Luhaga akionyeshwa kifaa
maalum cha kuchanjia mifugo wakati wa zoezi la ujanjaji wa mifugo
kitaifa pamoja na wataalam wa mifugo lililofanyika leo kwenye kijiji cha
Kinyangiri wilayani Mkalama mkoani Singida.

WAZIRI
wa Mifugo na Uvuvi (mwenye kofia nyeusi) Luhaga akihutubia umati wa
wadau wa mifugo wakati wa zoezi la ujanjaji wa mifugo kitaifa pamoja na
wataalam wa mifugo lililofanyika leo kwenye kijiji cha Kinyangiri
wilayani Mkalama mkoani Singida.

Umati
wa wadau wa mifugo wakati wa zoezi la uchanjaji wa mifugo kitaifa pamoja
na wataalam wa mifugo lililofanyika leo kwenye kijiji cha Kinyangiri
wilayani Mkalama mkoani Singida.


Na John Mapepele, singida

Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amesema Serikali inakusudia kuwezesha
kujenga kiwanda kikubwa cha kisasa cha kuchaka nyama ya kuku kwenye
Mkoa wa Singida kitakacholisha Tanzania na nchi mbalimbali duniani
ambacho kitakuwa kinafanya uzalishaji ifikapo Desemba mwaka huu ili
kuinua hali za wafugaji wa kuku wa Singida na kuongeza pato la taifa.

Mbali
na kiwanda hicho, Wizara ya Mifugo na Uvuvi inatarajia kujenga Kliniki
bora ya kisasa ya mifugo kwenye Halmashauri ya Mkalama. 

Kliniki
hiyo ni miongoni mwa Kliniki 30 ambazo zinazijengwa nchi nzima na
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli
kwenye Halmashauri mbalimbali.

Waziri Mpina
ameyasema haya kwenye hotuba yake ya uzinduzi wa Kampeni ya Chanjo za
Mifugo Kitaifa kwenye kijiji cha Kinyangiri katika Wilaya ya Makalama
mkoani Singida ambayo imelenga kutokomeza magonjwa mbalimbali ya mifugo
(hususan magonjwa 13 ya kipaombele) ambayo yamekuwa kikwazo katika
uzalishaji na biashara ya mifugo ndani na nje ya Tanzania.

“Tumeona
hapa uzalishaji mkubwa sana wa kuku Singida, sasa ninaagiza mambo
makubwa mawili Bodi ya Nyama na Dawati la linaloshughulikia Sekta
Binafsi katika Wizara yangu kuwezesha kujenga kiwanda cha kuchakata
nyama ya kuku na tutakizindua kikiwa kinatoa huduma ifikapo Desemba
mwaka huu”

“La
pili ninamuagiza Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko na Dawati la Sekta
Binafsi kuunda vikundi na kuwaletea vitotoleshi vya kisasa ili
kuongeza kasi ya uzalishaji wa kuku ili kuwezesha upatikanaji wa
malighafi za kiwanda kwa uhakika” alisisitiza Waziri Mpina.

Mpina
amesema magonjwa mengi ya mifugo ni yale ya kuambikiza hususani
yanayotokea kwa mlipuko na kusabisha vifo na hasara kubwa kwa wafugaji
na kufafanua kuwa hadi sasa tayari, Serikali imekiimarisha kiwanda cha
chanjo cha Tanzania Vaccine Institute (TVI) na kinazalisha aina sita
(6) ya chanjo za kipaumbele na kitaanza kuzalisha aina nyingine tatu
kufikia mwezi Desemba, 2020.

Mbali na Serikali kupitia Wizara
ya Mifugo na Uvuvi kuanza kutengeneza chanjo sita Mpina amesema
mapinduzi na mageuzi makubwa yamefanyika ili kuhakikisha kuwa Sekta ya
Mifugo inatoa mchango mkubwa katika uchumi wa nchi na kwa mwananchi
mmoja mmoja tofauti na awali ambapo sekta hiyo na wafugaji
walidharaulika sana.

Ametaja baadhi ya mambo yaliyoboreshwa
kwenye eneo la chanjo hapa nchini kuwa ni pamoja na Wizara yake
kupitisha Mpango wa Ununuzi wa Chanjo za Mifugo kwa Pamoja (Vaccine Bulk
Procurement Plan);

Serikali kutangaza Bei Elekezi ya chanjo
aina 13 za magonjwa ya kipaumbele ambapo chanjo zimepungua bei kwa zaidi
ya asilimia 60;

Amebainisha kuwa, Katika mwaka 2019/2020,
Serikali katika kiwanda cha TVI imezalisha jumla ya dozi 53,851,850 za
chanjo za magonjwa ya mlipuko na yanayovuka mipaka na chanjo hizi zote
zimechanja mifugo;

Pia, Wizara imevutia wawekezaji na kiwanda
kikubwa cha Hester Biosciences Africa Limited kinajengwa na
kitakapokamilika kitakuwa kinazalisha aina 37 ya chanjo za wanyama.

Ameongeza
kuwa katika mwaka 2019/2020, utoaji wa chanjo umeimarika ambapo
Halmashauri 103 kati ya 185 sawa na asilimia 56 zimeshiriki kikamilifu
katika kutoa chanjo kwa mifugo

Aidha Mpina amesema kutokana na
mikakati ya Wizara yake ya kudhibiti utoroshaji wa mifugo kutoka nchni
kwenda nchi za nje na udhibiti wa uingizaji holela wa bidhaa za mifugo
nchini kupitia “Operesheni Nzagamba” Serikali ya awamu wa Tano chini ya
Rais John Pombe Magufuli kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliweza
kukusanya zaidi ya bilioni 50 kwa mwaka ukilinganisha na Shilingi
bilioni 9.5 zilizokuwa zikikusanywa katika kipindi cha nyuma kwa mwaka.

Akitoa
maelekezo kwa wataalam Waziri Mpina amewataka wataalmu wote wa mifugo
ngazi ya Wizara, Mikoa, Wilaya na Kata kuhakikisha uchanjaji wa mifugo
unatekelezwa kikamilifu kulingana na kalenda ya chanjo kwa kuwa ni suala
la kisheria ambapo amemtaka Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo (DVS)
kuhakikisha unasimamia jukumu hili na yeye kupatiwa ripoti ya chanjo
hizo kila mwezi.

Pia amewataka Wataalamu wote wa mifugo
kuhakikisha wanatoa elimu ya chanjo kwa wafugaji ili watambue umuhimu na
faida za kuchanja mifugo yao na kwamba, Serikali imeshaandaa mazingira
wezeshi ya upatikanaji wa chanjo kila mahali na kwa bei elekezi.

Amesema
kulingana na Kalenda ya chanjo kitaifa, mwezi Juni mpaka Augosti, 2020
ni msimu wa chanjo za Homa ya Mapafu ya Ng’ombe, Homa ya Mapafu ya
Mbuzi, Sotoka ya Mbuzi na Kondoo, Ugonjwa wa kutupa mimba na Ugonjwa wa
Miguu na Midomo.

 Hivyo, ametoa wito kwa madaktari wa mifugo wote nchini kuhakikisha kwamba chanjo hizi zinatolewa kikamilifu.

Aidha
ameziagiza Halmashauri zote ambazo hazitowi huduma ya chanjo kwa mifugo
yao kufanya hivyo mara moja kuanzia mwezi huu wa Julai, 2020. 

Ripoti ya idadi ya mifugo na aina ya chanjo inayotolewa iwe inaletwa kwa Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo (DVS) kila wiki.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )