JESHI LA POLISI SINGIDA LAWEKA ULINZI MASAA 24 KUZUIA WATU KUPITA KATIKA MAZIWA YALIYOUNGANA

 Askari polisi wakiwa katika barabara ya Mwaja iliyofungwa baada ya maji kujaa kufuatia maziwa mawili kuungana kutokana na mafuriko.
 Ulinzi ukiimarishwa.
 Ulinzi ukiimarishwa.
 Wananchi wakiwa eneo la tukio.

Wananchi wakiwa eneo la tukio.


Na Ismail Luhamba, Singida
MAZIWA ya Kindai na SingidaMunangi yamegeuka na kuwa kivutio kikubwa Mkoani wa Singida na Mikoa ya jirani baada ya maziwa hayo kujaa maji na kuungana kufutia mvua kubwa inayonyesha mkoani humo.
Baada historia kujirudia kwa maziwa haya mawili ya Kindai na SingidaMunangi kuungana na kusababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara inayounganisha eneo la Mwaja na  Manispaa Singida na vijiji vya jirani.
Kufutia hali hiyo, Serikali Wilaya ya Singida kupitia  Jeshi la Polisi wilaya  limeamua kuimarisha ulinzi ili wananchi wasiendelee kuvuka kwenye barabara hiyo na kuhatarisha usalama wao. 
Jeshi la Polisi Wilaya ya Singida  limeimarisha ulinzi huo kwa ajili ya kutekeleza agizo la Mkuu wa Wilaya wa Singida Mhandisi Paskas Muragili alilotaka jeshi hilo kufanya hivyo kufutia baadhi ya wananchi kuendelea kuvuka kwenye maziwa hayo licha ya Serikali kukataza kufanya hivyo.
“Napenda kuwapongeza sana wananchi kwa kutii sheria bila shuruti kwani toka agizo limetolewa na Mkuu wetu wa wilaya juzi tumeendelea kuweka ulinzi usiku na mchana kwenye eneo hilo na sasa wananchi wote wanapita  barabara ya VETA na Mwaja ambayo inapitika vizuri” alisema Mkuu wa Polisi Wilaya ya Singida, Florence Mwenda.
CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )