International Istqaama Muslim Commuty Yatoamsaada Kwa Wafungwa Kahama

SALVATORY NTANDU

Jumuiya ya kiislamu ya  International  Istiqaama muslim Community  imetoa msaada ya vyakula mbalimbali kwa Wafungwa waliofunga katika Gereza la wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga ili kuwasaidia katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Akikabidhi Msaada huo Mei 9 mwaka 2020 kwa mkuu wa Gereza hilo, Misana Shigumha Katibu wa Masijd Alwahab  kahama,  Shekhe Ahmed  Haroun  Alnoobiy amesema msaada huo umetolewa na watu kutoka taifa la Oman kwaajili ya wafungwa na kuwataka kuendelea kuwaombea ili mwenyezi mungu aendelee kuwapa kheri zaidi.

 “Tumeleta kilo 200 za mchele, kilo 200 maharage ndoo saba za mafuta ya kula, na sukari kilo 100,tunaomba mpokee,ndugu zenu wa oman wamewakumbuka kwa msaada huu naombeni muendeleze dua katika kipindi hiki cha toba,”alisema Alnobiy.

Aliongeza kuwa Jumuiya hiyo hapa nchini inahusika na kuisaidia jamii  hususani yatima, masikini na wagonjwa ndio maana ikaamua  kuwasaidia wafungwa hao ili nao waweze kumrudia Mwenyezi Mungu kwa  kufanya toba katika kipindi hiki maalumu cha mwezi Mtukufu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Masijd Alwahab Kahama, Shekhe Mohamed Issa amewaomba wafungwa kuutumia mfungo huu wa  Mwezi wa Ramadhani kwa  kumwombea Rais, Dk John Pombe Magufuli ili Mwenyezi Mungu aendelea kumpa hekima za kuliongoza taifa kwa amani.

“Dumisheni dua ili Mwenyezi Mungu aweze kutuondelea janga la Corona ambalo linaendelea kuutikisa ulimwengu,tunaimani Allah atatukinga na kutuepusha dhidi ya COVID 19,”alisema Issa.

Akipokea Msaada huo kwa niaba ya Kamishana Jenerali wa Jeshi la Mageraza nchini,Mkuu wa Gereza hilo,Misana Shigumha ameishukuru jumuiya hiyo kwa msaada huo na kusema kuwa utawafikia wafungwa hao kwa wakati.

Sambamba na hilo Misana amesema kuwa katika jitihada ka kukabiliana na ugonjwa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona katika gereza hilo wanaendelea kuzngatia maelekezo yote yaliyotolewa na serikali ikiwa ni pamoja na kuzingatia unawaji wa mikono na upimaji wa joto kwa wafungwa,mahabusu na watu wengine wanaotembelea eneo hilo.
CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )