IKUNGI YATEMBEA NA FALSAFA YA RAIS JPM KWA ASILIMIA 100

 Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi mwenye miwani akiongea na akina
mama wafanya biashara ya viazi lishe   wa Kitongoji cha Kideka kijiji
cha Nkunikana kuhusu kuchukua tahadhari ya kujikinga na Corona-Covid 19
kulia Mkuu wa Wilaya ya Ikungi  Edward Mpogolo kushoto Mkurugenzi
Mtendaji Justice Kijazi

 Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi(mwenye miwani) akitoa 
 maelekezo  ya namna bora ya kufanya kazi katika kikundi kwa 
wakikundi   cha Jitume Vijana chenye vijana kumi katika kijiji Ikungi,
ambacho pia kilichopata mkopo wa shilingi milioni 25 kwa ajili ya mradi
wa kutengeneza matofali ya sementi kutoka katika Halmashauri ya Wilaya
ya Ikungi.. Mkopo huo ni Mkakati iliyojiwekea Halmashauri ya Ikungi wa
kudhibiti na kupambana na ugonjwa wa Covid-19 kwa kutoa mikopo hiyo
isiyo na riba kwa vijana ili waweze kujitenga na kujifungia na kuendelea
na uzalishaji  mifuko hiyo.Nyuma yake Kulia Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri hiyo Justice Kijazi, pembeni  kulia (mwenye koti jeusi) ni
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo

 Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi(mwenye miwani) akipata
maelekezo  kutoka kwa  katibu wa kikundi cha The New Bright Future – Petro Mwacha  jinsi
mashine ya kutengenezea mifuko mbadala  ya kikundi cha The New Bright
Future chenye vijana  10 waliopewa mkopo wa Milioni 25 na Halmashauri ya
Wilaya ya Ikungi mara  baada ya kuzindua kiwanda hicho. Mkopo huo  ni
Mkakati iliyojiwekea Halmashauri ya Ikungi wa kudhibiti na kupambana na
ugonjwa wa Covid-19 kwa kutoa mikopo hiyo isiyo na riba kwa vijana ili
waweze kujitenga na kujifungia na kuendelea na uzalishaji  mifuko
hiyo.Nyuma yake Kulia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Justice
Kijazi, Kulia (mwenye koti jeusi) ni Mkuu wa wilaya ya Ikungi Edward
Mpogolo

Mkuu
wa Mkoa wa  Singida(mwenye Miwani) akiuliza  maswali kwa  vijana
wanaotengeneza mifuko mbadala  ya kikundi cha The New Bright
Future(mwenye koti jeusi ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo,
Nyuma ya Mkuu wa Mkoa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Ikungi Justice Kijazi

Na John Mapepele, Singida


Falsafa ya Rais John Pombe Magufuli ya kutaka wananchi wake kuchukua
tahadhari zote zinazotolewa na wataalam wa afya za kudhibiti na
kujikinga na ugonjwa, wa Covid-19, kumwomba Mungu na kuendelea kuchapa
kazi ili kunusuru kupoteza maisha na kushuka kwa uchumi wa nchi yao
zimetekelezwa kwa vitendo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani
Singida.

Akitekeleza falsafa hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi
amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Ikungi na kuzindua kiwanda cha
kutengeneza mifuko mbadala katika Kijiji cha Siuyu Wilaya ya Ikungi.

Kiwanda hicho kilichoanzishwa kikundi cha New Bright Future chenye
vijana 10 waliopata mkopo usio na riba wa shilingi milioni 25 na Mradi
wa kutengeneza matofali ya sementi wa Kikundi cha Jitume Vijana chenye
vijana 10 kwenye Kijiji Ikungi ambacho pia kimepata milioni 25 kutoka
Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.

Ikiwa ni mkakati maalum wa kupambana na gonjwa la Covid-19 kwa kuwatenga
na kuwafungia vijana kwenye uzalishaji wa bidhaa badala ya kuzagaa
katika mikusanyiko isiyo ya lazima inayoweza kusambaza ugonjwa huo
kirahisi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Justice Kijazi, hadi sasa tayari Halmashauri imeshatoa jumla ya milioni
127 kwa wanufaika 78 ambapo inatarajia kutoa hadi milioni 150 kwenye
mwaka huu wa fedha endapo makusanyo yatakuwa kama yalivyokadiriwa

Dkt. Nchimbi amepongeza mikakati inayofanywa na Halmashauri ya Ikungi
kwa ubunifu na uratibu mzuri wa kutoa na kuelekeza mikopo kwenye miradi
ya viwanda vya uzalishaji bidhaa.

Ambapo amesema kwamba mkoa huo umeendelea kuweka mkakati wa kudumu wa
kujitenga na kujifungia katika maeneo mbalimbali ya uzalishaji ikiwa ni
pamoja na viwandani ili kuepukana na kuenea kwa ugonjwa wa Covid-19 na
kuongeza uzalishaji unaoendana na falsafa ya Mhe. Rais Magufuli wa
kuchapa kazi kwa bidii na kuendelea kuzingatia maelekezo ya wataalam
katika kipindi hiki.

Ameitaka Halmashauri ya Ikungi kutatua changamoto zote zinazokikabili
kikundi cha The New Bright Future ili kiweze kuzalisha kikamilifu na
kisaidiwe kupata masoko ya uhakika wa bidhaa zake ili fedha ya Serikali
iliyotolewa isipotee bali iwe na tija hatimaye iweze kurejeshwa na
kuwanufaisha wakopaji wengine

Aidha amezielekeza Halmashauri zote katika Mkoa wa Singida kuiga mfano
wa Halmashauri ya Ikungi katika utoaji wa mikopo inayoelekeza katika
uzalishaji wa bidhaa na viwanda na kupiga marufuku kutoa mikopo ya fedha
na kwamba mikopo lazima itolewe kwa kasi kama kasi ya maambukizi ya
ugonjwa wa Covid-19 ili wanavikundi hao wajitenge na kuendelea na
uzalishaji

Akiwa kwenye Soko maarufu la viazi lishe kwenye Kitongoji cha Kideka
katika Kijiji cha Nkunikana aliwapongeza wafanyabiashara hao kwa
kuzingatia maelekezo ya Serikali ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa
wa Covid-19 kwa kuandaa miundombinu ya maji ili kunawa mikono kwa sabuni
katika maji yanayotiririka wakati wote.

Mkuu huyo wa mkoa pia aliwataka wakulima wa viazi lishe kuendelea kulima
kwa bidii ili wananchi wapate lishe bora kutokana na viazi hivyo na
majani yake ambapo alisisitiza kuwa katika kipindi hiki ni muhimu
kusanitaizi mikono na kusanitaizi afya zao

“Naelekeza wakulima waache visingizio nao waendelee kwenda mashambani
kujitenga na kulima kwa bidii katika kipindi hiki ili waweze kupata
mazao mengi na wakati huo huo watekeleze matakwa ya Serikali ya
kujitenga na mikusanyiko isiyo ya lazima ambayo ingeweza kusababishia
maambukizi endapo mmoja ana maambukizi.”

Dkt. Nchimbi amesema ugonjwa Covid-19 uwe ni chachu ya kufanya kazi kwa
bidii za uzalishaji na kwamba viwanda hivyo viwe darasa maalum ya
kutolea mafunzo hayo bila malipo kwa vijana wengine ili kuwapa maarifa
kwa vijana wengi zaidi

Katika uzinduzi huo mkoa huo ulitoa kiasi cha shilingi milioni moja huku
Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ikitoa kiasi cha shilingi milioni tano
na kufanya jumla ya shilingi milioni 6 zilizoombwa na kikundi cha The
New Bright Future kwa ajili ya kununua malighafi kupatikana.

Katika hatua nyengine Mkuu wa Mkoa alielekeza Serikali ya Wilaya ndani
ya kipindi cha mwezi mmoja kutumia jengo jingine la Kijiji cha Isuna
katika Wilaya ya Ikungi ambalo ni mali ya Serikali kwa vikundi vya
uzalishaji ambalo kwa sasa halitumiki kwa shughuli yoyote ile.

Akisoma hotuba mbele ya Mkuu wa Mkoa Katibu wa kikundi cha The New
Bright Future Petro Mwacha ameishukuru Serikali kwa kuwapa mkopo huo na
kusisitiza kuwa mradi huu umelenga kuunga mkono juhudi na kauli mbiu za
Rais, John Pombe Magufuli za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa
kati wa viwanda ifikapo mwaka 2025.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo alisema Serikali ya Wilaya
tayari imejipanga vizuri kujikinga na ugonjwa huo ambapo hadi sasa elimu
ya ugonjwa wa Covid-19 kwenye maeneo mbalimbali inaendelea kutolewa.

Amesema Wilaya ya Ikungi ni miongoni mwa Wilaya ambazo zipo katikati ya
nchi ya Tanzania ambapo barabara kuu inayounganisha mikoa na nchi
mbalimbali na kwamba mwingiliano wa watu ni mkubwa, hivyo njia bora ya
kukabiliana na ugonjwa huu ni wakuwatenga watu kwa kutumia mkakati
maalum wa kuwapa mikopo ambayo itawafanya wananchi wajifungie na
waendelee na uzalishaji huku wakichukua tahadhari zote za kujikinga
zinazotolewa na wataalam wa afya.

Share:
CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )