Ikizu Pharmacy watoa msaada wa Vifaa Kinga kwa Waandishi wa Habari.

Na John Walter-Babati
Mdau wa Maendeleo mkoa wa
Manyara (IKIZU PHARMACY) ambayo inashughulika na kutoa huduma za afya kwa kuuza
dawa za Binadamu, ametoa msaada wa vifaa vya kinga vya corona kwa waandishi wa
Habari mkoa wa Manyara.
Akitoa msaada huo mwakilishi
kutoka Ikizu Pharmacy Wilson Mbogo,  amesema
wameamua kuwapatia waandishi wa habari msaada huo ili waweze kufanya kazi zao
kwa uhuru na salama.
Mbogo amesema kuwa msaada
walioutoa kwa ajili ya kuwasaidia waandishi wa habari katika kipindi hiki cha
mlipuko wa homa ya mapafu (COVID19) una thamani ya shilingi laki sita na sitini
elfu.
Mwenyekiti wa Klabu ya
waandishi wa Habari mkoa wa Manyara Yusufu Daiy amesema misaada walioipokea ni Vitakasa
Mikono,Sabuni za mikono,Gloves pamoja na barakoa.
Katibu wa Klabu ya waandishi
wa Habari mkoa wa Manyara (MANYARA PRESS CLUB) Thedy Challe amemshukuru mdau
huyo huku akiahidi kugawa msaada huo kwa waandishi kama ilivyokusudiwa.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )