IGP Simon Sirro atoa maelekezo mazito kwa wakuu wa police wa wilaya.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro
amewaagiza Wakuu wa Polisi wa Wilaya OCDs kuhakikisha wanasimamia mikutano
wakati wa kampeni ili iwe ya amani na utulivu.

IGP Sirro amesema hayo leo akiwa mkoani Simiyu
wakati alipofanya ziara ya ukaguzi katika mkoa huo na kuzungumza na maofisa na
askari wa Jeshi hilo ambapo alisema kuwa Jeshi la Polisi limejipanga kusimamia
uchaguzi na kwamba litaendelea kutoa elimu kwa wananchi ikiwa pamoja na
kushirikiana ipasavyo na wadau wa uchaguzi.


Aidha, IGP Sirro amewapandisha vyeo askari
wawili wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia FFU mkoa wa Simiyu kutoa cheo cha konstebo
wa Polisi na kuwa Koplo wa Polisi kutokana na umahili wao wa kutekeleza
majukumu wanayopewa.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )