HOFU YA VIRUSI VYA CORONA RC CHALAMILA AAGIZA WILAYA KUWA NA KARANTINI

Na Esther Macha, Mbeya
MKUU wa Mkoa wa Mbeya , Albert Chalamila  amesema kuwa  katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa corona wilaya zote zimeagizwa kuwa  na kantini ya kuhifadhi watu watakaobainika kuwa na dalili  na kwamba tayari serikali mkoani hapa imepokea dawa na vifaa tiba vya kutosha kutoka katika Bohari ya Dawa (MSD).

Chalamila aliyasema hayo jana wakati akipokea vifaa hivyo kutoka Bohari ya Dawa pamoja na kutembelea maeneo ya vituo vya afya yaliyotengwa kwa ajili ya kuhifadhi watu watakaobainika na dalili.

” Kwa sasa Serikali tumejianga  kikamilifu katika mipaka yetu ili kuhakikisha raia wote wa kigeni wanaoingia nchini wanapimwa joto na vifaa maalum ili kuweza kudhibiti maambukizi  ya  corona  na kuimarisha ulinzi katika   mpaka yetu na kudhibiti njia za kipanya “alisema.

Hata hivyo Mkuu huyo wa mkoa alisema  raia tisa wa kigeni  wamehifadhiwa kwenye kantini wakiwa katika  uangalizi maalum na kufanyiwa vipimo ndani ya siku 14   ili kubaini kama wanaviashiria vya maambukizi ya  ugonjwa wa  homa ya corona.

Aidha Chaamila alisema zaidi ya 150 milioni za raia wa wakigeni waliongia nchini kinyume cha sheria zimetaifishwa  na Serikali mkoani hapa .

Katika hatua nyingine akiwa katika kituo kikuu cha mabasi ya Mikoani Chalamila ameonya vijana kuachana na tabia ya kuboresha mapenzi kwa kunyonyana ulimi na kwamba hiyo ni hatari kubwa inayoweza kusababisha magonjwa mbalimbali ikiwepo corona.

“Vijana nawaonya acheni tabia hiyo mara moja kwani kuna baadhi yenu bila kupeana ulimi   ni kunogesha upendo upendo hata bila kupeana ulimi inawezekana tu shirikianeni na Serikali kupinga corona kwa kuepuka tabia hatarishi “alisema.

Aidha kwa upande mwingine aliwaondoa hofu wafanyabishara kuwa serikali haitoweza kuwafungai katika biashara za  kumbi za starehe,mamalishe, na  maduka ya pombe na badala yake wafanyabishara wazingatia kanuzi za afya kwa kila mmoja kwa nafasi yake kuwa na maji miminika na sabuni yenye dawa.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya  Jiji la Mbeya , James Kasusura ameagiza mabasi yote yanayotoka na kuingia katika vituo vya mabasi kuwa na sabuni yenye dawa na maji tililisha ikiwa ni pamoja na pikipiki za mataili matatau (bajaji) bodaboda na tax.

Alisema hilo ni agizo na lazima litekelezwe  na kufanya ufuatiliaji na watakaobainika kutofanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa sambamba na kuwataka wananchi kuwafichua ili kuweza kuunga mkono jitihada za serikali kupiga vita ugonjwa wa corona.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya , William Ntinika alisema kuwa  jamii imeonyesha mwamko mkubwa wa kujikinga ikiwa ni kwenye migahawa, maduka ya pombe, na kumbi za starehe.

Ntinika alionya wananchi kuachana na dhana  ya kuuchukulia ugonjwa huo kama ni wakutisha na kuchangia jamii kujenga hofu na kwamba ufike wakati kutii sheria bila shuruti kwa kutokuwa kwenye mikusanyiko ya watu wengi  ili kukabiliana na changamoto na maambukizi ya corona.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )