HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA YAMPONGEZA RAIS JPM KWA HATUA ALIZOCHUKUA KUKABILIANA NA COVID 19
 Kaimu Ofisa Afya wa Jiji la Tanga Hamza Maulidi akizungumza wakati akitoa elimu katika semina ya siku mbili  inayotolewa kwa Wasaidizi wa msaada wa kisheria (Paralegals) kutoka halmashauri 11 zilizopo mkoani Tanga,


 Kaimu Ofisa Afya wa Jiji la Tanga Hamza Maulidi akizungumza wakati akitoa elimu katika semina ya siku mbili  inayotolewa kwa Wasaidizi wa msaada wa kisheria (Paralegals) kutoka halmashauri 11 zilizopo mkoani Tanga


 Programu Meneja wa Shirika la TEWOREC Halima Jabiri Saguti akisisitiza jambo jana wakati akitoa elimu ya msaada wa
kisheria kwa wasaidizi wa kisheria Mkoani Tanga yaliyoendeshwa na
Shirika hilo Jijini Tanga kwa kushirikisha wilaya zote za mkoa huo


 AFISA wa Tathimini na Ufuatiliaji wa Taasisi ya TEWOREC akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo


 Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Majira Mashaka Mhando akitoa uzoefu wake wakati wa semina hiyo

 Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akichangia

HALMASHAURI ya Jiji la Tanga, imempongeza Rais John Magufuli, kwa hatua alizochukua kukabiliana na ugonjwa wa Corona nchini.

Sambamba
na pongezi hizo, ugonjwa huo katika Jiji la Tanga unapungua kwa kasi
kutokana na wananchi wengi kuchukua tahadhari zinazotolewa na Serikali
pamoja na wataalamu wa afya.

Akizungumza kwenye semina ya siku
mbili inayotolewa kwa Wasaidizi wa msaada wa kisheria (Paralegals)
kutoka halmashauri 11 zilizopo mkoani Tanga, Kaimu Ofisa Afya wa Jiji la
Tanga Hamza Maulidi alisema wananchi hawana budi kumpongeza Rais kutoka
na kututoa hofu tangu alipogundulika mgonjwa mmoja hapa nchini.

Alisema
kweli ugonjwa huo bado upo nchini na wananchi waendelee kuchukua
tahadhari zote pamoja na kwamba maambukizi yanashuka kwa kasi kubwa
Jijini hapa, lakini pia wanampongeza Rais kwa hatua alizochukua hadi
ugonjwa unaendelea kupungua.

“Ugonjwa upo na Tanga pia upo,
tuchukue hatua tunazoelekezwa na wataalamu wetu wa afya, lakini kwa
kweli tunampongeza mheshimiwa Rais kwa kututia faraja tangu ugonjwa huu
umeanza,” alisema Maulidi.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo
walisema yametolewa wakati muafaka ambao shughuli za kiserikali nyingi
zimeanza kufanyika baada ya mikusanyiko kuzuia hivyo itawasaidia kupata
uelewa mkubwa wa ugonjwa huo na taadhari zake.

Awali akifungua
mafunzo hayo Meneja wa Shirika la kutoa msaada wa kisheria mkoani Tanga
(TAWOREC) Halima Saguti alisema lengo la kutoa mafunzo kwa Paralegal hao
ni kutaka wanapotoa huduma kwa wananchi huko vijijini waweze kujiinga
na maambukizi ya ugonjwa huo.

Alisema kazi za wasaidizi hao wa
kisheria zimekuwa zikiendelea huko vijijini na hivyo kupewa elimu hiyo
kutasaidia kupunguza kusambaa kwa ugonjwa huo kwa watu wengine.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )