HALI YA USAJI,UTUNZAJI WA KUMKUMBUKU YA VIZAZI NCHINI BADO HAIRIDHISHI

KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Judica Omari akizungumza wakati akifungua semina ya viongozi wa mkoa na wilaya zake kuhusu  usajili wa watoto
walio na umri chini ya miaka mitano kilichofanyika katika ukumbi mkuu
wa mkoa wa Tanga.


Kaimu
Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi
na Udhamini (RITA) Emmy Hudson akizungumza wakati wa semina hiyoMKURUGENZI Msaidizi Huduma za Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais Tamisemi Rasheed Maftah akizungumza wakati wa semina hiyo

Meza
kuu wakifuatilia matukio mbalimbali kutoka kushoto ni MKURUGENZI
Msaidizi Huduma za Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais Tamisemi Rasheed Maftah
akifuatiwa na Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) Emmy Hudson,Katibu Tawala
wa Mkoa wa Tanga Judica Omari na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Jonathan
Budemu
Katibu
tawala wa wilaya ya Korogwe Rahel Mhando kulia akifuatilia kwa umakini
semina hiyo akiwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Handeni Mashaka Mgeta
katikati na Katibu tawala wa wilaya ya Muheza Desderia Haule


MKUU
wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya ya
Tanga Thobias Mwilapwa wakifuatilia kwa umakini semina hiyo
MKUU
wa wilaya ya Lushoto January Lugangika kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya
ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia wakiwa kwenye semina hiyo KATIBU
Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange kushoto akiwa na
Katibu tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim kulia ni Mkurugenzi wa
Halmashauri ya wilaya ya Kilindi wakiwa kwenye semina hiy


 MKUU
wa wilaya ya Handeni Toba Nguvila kulia akiwa na Mkuu wa wilaya ya
Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo wakifuatilia matukio mbalimbali


Katibu Tawala wa wilaya ya Mkinga Joseph Sura akifuatilia kwa umakini semina hiyo Sehemu ya viongozi wa dini wakifuatilia semina hiyo


KUTOKANA
na ongezeko la mahitaji na matumizi ya cheti cha kuzaliwa nchini, hali
ya usajili na utunzaji wa kumbukumbu ya vizazi bado hairidhishi jambo
linalosababisha serikali kukosa takwimu sahihi kwa ajili ya mipango
mbalimbali ya maendeleo kwa Taifa ikiwemo elimu,afya na huduma nyengine
za msingi .

Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) Emmy Hudson ameyasema hayo
katika semina ya viongozi wa mkoa na wilaya zake kuhusu  usajili wa
watoto walio na umri chini ya miaka mitano kilichofanyika katika ukumbi
mkuu wa mkoa wa Tanga.

Hudson alisema alisema kwa mujibu wa
takwimu ya sensa ya 2012 ni asilimia 13 tu ya wananchi wa Tanzania Bara
waliosajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa hivyo kuifanya kuwa moja
kati ya nchi zenye kiwango cha chini cha usajili barani Afrika.

“Hii
ni changamoto ambayo serikali kupitia RITA kama Taasisi yenye dhamana
ya Usajili wa matukio muhimu ya binadamu kwa kwa kushirikiana na wadau
wengine tumechukua hatua stahiki kwa kuandaa mkakati wenye lengo la
kukabiliana na changamoto hii” amesema Hudaon.

Hata hivyo
amebainisha kwamba tayari hatua madhubuti zimechukuliwa ili kukabiliana
na changamoto hiyo kwa kufanya maboresho ya ujumla ya mfumo mzima wa
usajili chini ya mkakati wa kitaifa na kuboresha Usajili wa matukio
muhimu ya binadamu na takwimu. 

Alisema
mkakati huo umeandaliwa baada ya kufanyika kwa tathimini ya kina na
kubaini mapungufu katika mfumo wa usajili uliopo huku akieleza mpango
huo wa Taifa wa kuboresha usajili na matukio muhimu ya binadamu na
takwimu umebeba mipango mbalimbali ya utekelezaji ikiwa ni ya muda mfupi
na mrefu ukilinganisha na makundi makuu matatu yanayotokana na umri ili
kufikia makusudio ya usajili.

Aidha alisema kundi la kwanza ni
watoto wa umri chini ya miaka mitano ambapo serikali kwa kushirikiana na
wadau wa maendeleo imebuni mpango wa usajili na kutoa vyeti vya
kuzaliwa kwa watoto wa kundi hilo.

“Tayari mpango huu unaendelea
kutekelezwa katika mikoa kumi na sita ya Mwanza,
Mbeya,Songwe,Iringa,Njombe,Geita,Shinyanga,Mtwara,Lindi,Mara,Simiyu,Dodoma,Singida,Morogoro,Pwani
na Ruvuma na kuonyesha mafanikio chanya hivyo kikao hiki ni maandalizi
ya kuanza utekelezaji katika mkoa wa Tanga “Alisema

Awali
akizungumza wakati akifungua semina hiyo Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga
(RAS) Judica Omari ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine
Shigella alisema maisha ya mwanadamu yanaanzia pale anapozaliwa hivyo
basi tukio la kizazi maana yake ni kuongezeka kwa idadi ya watu katika
jamii na Taifa kwa upande wao kama serikali inawakumbusha wajibu wa
kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi.

Alisema kwa mantiki hiyo
usajili na upatikanaji, utunzaji wa kumbukumbu sahihi kila tukio jipya
la kizazi linapotokea ni la msingi kuweza kutambulika kwani kufanya
hivyo kutaweza kuwa na uhakika wa kuweka takwimu sahihi kwa wakati na
kupunguza matumizi ya takwimu za makisio ambazo zote wanazifahamu
changamoto zake.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )