FLORAH MAGABE AMUUNGA MKONO MHE. MAGUFULI KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA CORONA COVID-19

Mjumbe wa halmashauri Kuu Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza Bi. Florah Magabe hivi leo amekabidhi Vitakasa Mkono na Sabuni Lita 200  pamoja na Tank Saba za Maji zenye uwezo wa kuhifadhi Lita 1,750 kwa uongozi wa CCM mkoa wa Mwanza kwaajili ya kujikinga na homa ya Mapafu inayotokana na Kirusi Cha Corona Covid-19.

Akipokea msaada huo Comrade Salum Kalli Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza amesema Mkoa wa Mwanza unakata 191, matawi 917 pamoja na mashina 13,230 ambayo yote yanaendelea na kazi Kama kawaida  hivyo, amepongezi Kwa Bi.  Magabe kwa msaada huo katika wilaya Saba ambao utawawahakikishia usalama kazini watumishi pamoja na wananchi wanaofuata huduma.

Naye Bi. Magabe akikabidhi Msaada amesema, amewiwa kukisaidia Chama Cha Mapinduzi wilaya zote Saba za Mwanza pamoja na Jumuiya zote ngazi ya Mkoa kwa maana CCM ndio chama pekee ambacho kinaishi farsafa ya Mwenyekiti wa CCM taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ya *Hapa Kazi tu* kwa kuchapa Kazi kwa vitendo. Hivyo watendaji hao wakiwa kazini na wananchi wakifuata huduma waendele kujikinga  homa ya Mapafu inayotokana na Kirusi Cha Corona Covid-19 kwa kunawa Mikono na maji Tiririka na Sabuni.

Hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika ofisi za CCM Mkoa wa Mwanza na kuhudhuriwa na Secretariet ya CCM Mkoa, Mwenyekiti wa Chipukizi Mkoa wa Mwanza Bi. Marie-Kighei Kahungwa pamoja na Mwenyekiti wa Vyuo Vikuu Semeti Mkoa wa Mwanza.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )