Fahamu Mchango wa marafiki katika maisha yako


Kuna aina mbili za marafiki ambao tunaishi nao katika maisha yetu ya kila siku.  Aina ya kwanza ni marafiki ambao ni wema na aina ya pili ni marafiki wabaya.

Tukianza na kuangalia aina hiyo  ya kwanza, marafiki wema  ni marafiki ambao ni watu ambao wana mawazo chanya katika kukushauri hata kutenda mambo mbalimbali yenye mchango mkubwa wa kuyabadili maisha yako kwa kiwango cha juu sana. Pia katika kundi hili la marafiki  wema ni wapo wachache sana.

 Aina ya pili, marafiki wabaya hawa ni  marafiki ambao ni watu ambao hawana msaada wowote katika safari yako ya mafanikio zaidi ya kukukatisha tamaa tu. Aina hii ya marafiki hawapo tayari kukusaidia katika shida bali wapo kwa ajili ya raha pekee.

Pamoja na hayo watu wengi tunafeli kimaisha hii ni kutokana na kufanya uchaguzi mbaya wa marafiki. Wengi wetu tunaambatana na marafiki wabaya hata sehemu ambazo hatustili kuishi na watu hao .

Vile vile wengi wetu tumekuwa tukiomba ushauri kwa watu ambao siyo sahihi hata kidogo. Kwa mfano leo hii tumeona marafiki wabaya huwa na mtazamo mmoja wa kushindwa kufikia malengo yao nay a watu wengine.
Tumekuwa tukishuhudia  baadhi ya wanafunzi ambao pindi waendapo  masomoni baada ya kufika huko wamekuwa  wakibadilika sana tabia zao, wengi wao wamekuwa na  tabia za ajabu sana, hii ni kutokana wamekutana na marafiki ambao sio sahihi kwao ni wao kutokana na ufinyu wa fikra walizonazo wamejiunga nao.

Tumeona baadhi ya vijana hao wamekuwa wakijingingiza kwenye wimbi la ulevi,  utumiaji wa madawa ya kulevya na hata kuuza miili yao hii ni kutokana watu hao wameshindwa kuchagua marafiki sahihi.

Achilia mbali wanafunzi, Wapo baadhi ya watu wameshindwa kuwa sehemu fulani kwa sababu ya marafiki walio nao. Wapo baadhi ya watu wamekuwa wakipata baadhi ya mawazo mazuri yenye kuleta mapinduzi katika maisha yao na jamii kwa ujumla, ila wamekuwa wakiwashirikisha marafiki zao mawazo hayo kabla ya kuyaamua kuyafanyia kazi, na marafiki hao  wabaya walio nao baadala ya kuwapa ushauri mwema wamekuwa wanazidi kuwakatisha tamaa tu.

Neno haiwezikani ndilo linalowaongoza wao kwa silimia kubwa, Kwa mfano unaweza ukamshirikisha rafiki yako kuwa unataka kufanya biashara ya fulani. Baada ya kumwambia rafiki huyu uliyenaye utamsikia akisema Biashara hiyo haitatoka kwa sabubu fulani  naye anaifanya au fulani kaliteka soko la biahara hiyo, hivyo  wewe hatuweza ni bora utafute kitu kingine cha kufanya. Kwa kuwa na wewe muoga na unaamini katika maneno ya kuambiwa unajikuta unaacha. Kwa staili hiyo akama endapo hutaamua leo kubadilika ni kwamba neno mafanikio utaendelea kulisikia tu.

Hii ni kwa sababu ukichunguza kwa umakini juu ya marafiki wabaya huwa hawana sababu ya msingi ya jambo ambalo anakwambia kwa nini usifanye zaidi ya kukwambia usifanye tu.

Vile vile wapo baadhi ya marafiki ambao wao pia ukiwashirikisha jambo lako na wao huchukua jukumu la kuwashirikisha wengine. Marafiki wa aina hiyo hawafai hata kidogo.

Kimsingi ni kwamba watu wengi walio fanikiwa leo hii walichagua marafiki sahihi wa kuwashauri juu ya mambo yao. Hivyo na wewe chagua marafiki sahihi ambao unahisi wanamsaada mkubwa katika maisha yako, pia ukumbuke  msemo usemao ndege wafananao huruka pamoja hivyo ni wasaa wako mzuri wa kuchagua marafiki wema kwako. Marafiki wabaya ambao hawana mchango na msaada wowote juu ya maisha yao wafute na wala usijali watesema nini.

Marafiki hao wabaya wakianza kukuliza kwanini siku hizi umebadilika jibu la kuwajibu ni rahisi ni kwamba utawaambia “always forward, backward never” ikiwa na maana ya daima mbele, nyuma mwiko.
Chagua marafiki sahihi ambao wao ukiwaambia juu ya jambo lako zuri tegemea kupata majibu sahihi pia kwa kile ulichowashirikisha na sababu za msingi.

Pia kumbuka usemi usemao ya kwamba kila gumu unalokutana nalo mbele yako limebeba siri ya mafanikio yako, usinung’unike kutokana na magumu unayokutana nayo katika mizunguko yako lakini ifundishe akili yako, usingalie nani kasema nini? nani kasema kipi juu yako. Jambo la msingi ni fanya kazi kwa bidii zote na simamia mipango yako . Siku moja utakuwa mtu wa thamani sana mbele ya jamii.

Ndimi Ofisa Mipango na Maendeleo: Benson Chonya

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )