Fahamu Jinsi ya kuongeza ufanisi wa kiutendaji katika kazi yako

Ili uweze kuwa bora katika kazi hatimaye upate matokeo chanya unatakiwa kuelewa mambo yatakayokusaidia kuweza kuwa hivyo. Kila kitu unachokiona leo hii mbele ya mboni ya jicho lako elewa kuwa mmliki wa kitu au jambo hilo aliweza kujifunza namna ya kuweza kukifanya kitu au kitu chake kiweze kuwa bora.

Hivyo ili na wewe uweze kuongeza ufanisi katika kazi unayoifanya ili uweze kufanya kitu au jambo lenye ubora unatakiwa kuzingatia mambo yafutayo;


Unatakiwa kutenga muda wa kujifunza.
Hakuna kitu kinachokuwa bora kwa miujiza. Kitu chochote ili kiweze kuwa bora ni lazima muhisika wa jambo hilo aweze kuwekeza muda mwingi wa kujifunza juu ya jambo hilo.

Kama unafanya biashara unashauriwa kutoridhika na kile unachokipata pekee, bali ili uweze kupata zaidi unatakiwa kujifunza zaidi ya kuongeza mauzo yako. Watalamu wa mambo wanasema kiwa kujifunza hakuna ukomo, hivyo kwa kila kitu unachokifanya ni vyema ukahakikisha kwamba kwa kila kitu unachokifanya ili kiwe bora na hatimaye upate matokeo chanya huna budi kujifunza kila siku juu ya jambo hilo.

Unashauriwa kujifunza kila kitu kwa sababu hizi ni zama za kisasa mambo yamekuwa yakibadilika sana, pia washindani ni wengi na wanazaliwa kila siku hivyo usipowekeza muda wako mwingi katika kujifunza ni kwamba wewe hautakuwa na utabaki vilevile kila siku hivyo unatakiwa  kujifunza kila wakati ili uweze kwenda sawa na ulimwengu wa sasa.

Jifunze kupangalia kazi zako.
Kitu chenye mpangilip ndicho chenye matokeo chanya siku zote. Ili uweze kuongeza ufanisi kwa kila kitu unachokifanya unatakiwa kuelewa namna ya kufanya mpangilio katika kazi zako.

Usikurupe kitandani mwako kama huelewi siku yako itaisha vipi. Bali unatakiwa kupanga ratiba yako katika mtiririko unaoeleweka. Katika hili panga nini unatakiwa kufanya na ndani ya muda gani, kufanya hivi itakusidia sana kuweza kufanya kazi zako kwa wakati pia inakusaidia kutokutoka nje ya malengo yako ambayo umejipangia kuyatekeleza katika siku yako.

Jambo hili la kupanga mtiririko wa kazi ni muhimu sana zaidi hata kula, hapa nimeweka chumvi kidogo ila huo ndiyo ukweli halisi.

Jifunze kuwa mmalizaji wa kazi zako.
Kila kitu ili kiwe bora kinatakiwa kumalizika katika kiwango cha ubora. Huwezi kusema unataka kuwa bora katika kazi zako wakati kila kazi unayoianzisha huwa haimaliki.

Ukiona unaanzisha kazi fulani harafu fulani kazi hiyo haimaliki basi ujue hilo ni Pepo hii ni kwa mujibu wa muimbaji fulani wa nyimbo za Injili. Ili uweze kuondokana na pepo hilo hatimaye kuapata matokeo chanya kwa kile unachokifanya unatakiwa kukimaliza kile unachokufinya.

Pindi utakapokuwa na visingizio visivyokuwa vya msingi husasani  katika jambo ulifanyalo elewa kuwa kila kitu unachokifanya kitakuwa kinaishia katika hatua za awali pekee. Hivyo naomba nikusiki ya kwamba kila kitu unachokifanya hakikisha pindi unapoanza kukufanya ni kwamba unakimaliza kitu hicho.

Epuka mrundikano wa kazi.
Hili ni jambo la muhimu sana katika ulimwengu wa mafanikio. Kama tulivyoona katika pointi iliyopita basi hapa unashauriwa kuepeuka mrundikano wa kazi, pindi utakapo zipangilia kazi zako basi elewa na namna ya kutimiza kazi kwa wakati ili uepuka mlundikano wa kazi.

Miongoni mwa faida utakazozipata pindi utakapokuwa na utaratibu wa kufanya kazi kwa wakati ni pamoja na kupunguza mrundikano wa kazi ambazo unatakiwa kuzifanya.

Hivyo nakushauri ewe msaka mafanikio ya kwamba unatakiwa kufanya kazi zako kwa wakati ili upate ya kweli.

Pata msimamizi.
Kila kitu ili kuweze kuwa bora kinahitaji kuwa na msimamizi, kama unajenga nyumba na huna msimamizi ambaye anaeleweka ni kwamba nyumba hiyo haitakuwa imara. Si kwenye nyumba huo umetumiaka kama mfano tu ila ukweli ni kwamba pindi utakapokuwa na msimamizi bora wa kazi zako utakuwa na maendelo ya kweli. Msimamizi ni mtu muhimu sana katika kila jambo ulifanyalo.

Jiulize maswali.
Ili kuwa bora zaidi katika kazi yako ni kwamba unatakiwa kujiuliza maswali, maswali haya ni lazima yalenge ni wapi umetoka, ni wapi ulipo na ni wapi unapokwenda, Kufanya hivi kutakusidia sana kupanga mweleko wa mafanikio yako husasani kile unachokipata.

Wajue washindani wako.
Kuwajuwa washindani wako ni njia nyingine ya kuongeza ufanisi wa kiutendaji katika kazi zako.  Kuwajua washindani wako inakusaidia sana kujua namna ya kuwashinda  hao washindani  kwa kile ukifanyacho hii ni kwa sababu utakuwa umejua mbinu wanazotumia washindani wako na wewe utakuwa umejua namna ambavyo utawapiku washindani hao.

Mafanikio ni haki yako ya msingi hivyo Ili uweze kupata matokeo chanya  wa kazi yako ni vyema ukahakikisha unayazingatia hayo kila wakati.

Na. Benson Chonya.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )