Elimisha inavyotabiri Tanzania kupata wageni wengi kimataifa.

Na Joachim Nyambo,Mbeya.

TANZANIA imeshauriwa kujiandaa kupokea
wageni kutoka mataifa mbalimbali duniani watakaokuja kwaajili ya kujionea
maajabu mbalimbali yanayoendelea kutokea nchini ikiwemo maamuzi magumu na yenye
tija ya Rais John Magufuli.
Miongoni mwa mambo yanayotajwa kuwa
kivutio kwa wageni kutoka mataifa ya mbali ni pamoja na maamuzi aliyoyafanya
rais Magufuli ya kutowafungia ndani wananchi kutokana na ugonjwa wa Homa kali
ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona maamuzi aliyoyasimamia mpaka
maambukizi yanatajwa kupungua kwa kasi nchini.
Ushauri huo ulitolewa na Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Elimisha Tanzania lenye makao yake makuu jijini
Mbeya,Festo Sikagonamo alipozungumzia utendaji kazi wa Serikali ya awamu ya
tano chini ya rais Magufuli.
Sikagonamo alisema mambo yaliyofanywa na
Magufuli ni makubwa na yanamtofautisha na viongozi  wengine Duniani
jambo linaloonekana kuzua gumzo katika mataifa mbalimbali yakiwemo makubwa na
yenye kupenda kunyenyekewa siku zote.
Alisema sababu hiyo itaifanya Tanzania
kupokea wageni wengi zaidi kutoka mataifa mbalimbali duniani ambao watakuja
nchini si tu kwa ajili ya kuangalia vivutio vya utalii vilivyopo bali wengine
watakuja kuifahamu Tanzania ilivyo sambamba na utawala wake.
“Wengine watakuja wakiwa na shauku kubwa
ya kutaka kumwona mubashara Rais Magufuli… kwamba ni mtu wa namna gani…ana
fananaje kutokana na mambo mazuri makubwa anayoyafanya kwa ajili ya taifa la
Tanzania.”alisema Sikagonamo
“Rais Dkt. John Magufuli ametumia fikra
bunifu na za kipekee kwanza kwa kuifanya Corona kama vita na sio janga la
kiafya linalohitaji mashauri ya kisayansi.Haya yalikuwa maono ya kitofauti
ikifananishwa na viongozi wa mataifa mengine”aliongeza.
Mkurugenzi huyo alimtaja Rais Magufuli
kuwa wa kipekee ulimwenguni ambaye alitumia mbinu bunifu na za kipekee kwa
namna alivyofanya uchunguzi katika maabara ya kitaifa jambo lililoyasaidia pia
mataifa mengine kufikiri mbali ya mitazamo yao ya awali.
“Ni rais Magufuli pekee ambaye hakutaka
kuiga au kuingia mkumbo wa nchi nyingine kwa kuwafungia watu ndani bali aliwatoa
hofu wananchi na aliwasisitiza kufanya kazi ili kuendeleza uzalishaji.Licha ya
mashirika ya kimataifa na nchi kubwa duniani kuitishia Tanzania kuitaka ifungie
watu, lakini kamwe Magufuli hakuteteleka.”alisema.
Alisema jambo lililozidi kuwapa moyo watanzania
na kuwaondoa shaka waliyokuwa nayo awali baada ya kuona rais wao anakwenda
tofauti na viongozi wengine ni pale Magufuli alipousaajabisha ulimwengu kwa
kutabili mambo mbalimbali ambayo baadye yalikuja kuigwa na Shirika la Afya
Duniani (WHO).
Aliongeza kuwa kutokana na msimamo wake
rais Magufuli amepunguza tishio la ugonjwa wa Corona na kuhamasisha utumiaji wa
tiba za asilia kama vile kunywa tangawizi na chai ya limao, na tiba ya kufukiza
kama njia ya kuzuia kuambukizwa kwa COVID 19.
Aliitaja pia hatua ya Tanzania kupeleka
ndege Madaska kuchukua Dawa kwa ajili ya kuifanyia utafiti ili kuweza kusaidia
watu wake kuwa ya kijasiri na yenye kulenga misimamo ya kutetea watu wake kwa
njia zinazoonekana zinafaa kwa maamuzi ya Taifa husika badala ya kusubiri
mataifa yanayojiona ndiyo wasemaji na wenye maamuzi ya mwisho.
Hatua ya Rais magufuli kuwa wa kwanza
kufungua safari za anga ili kuruhusu ndege za kimataifa kutua nchini Tanzania
aliitaja kuwa yenye kulenga zaidi maslahi ya Taifa kwakuwa kufanya hivyo
kunazidi kuwapa moyo wa kufanya kazi kwa kujittuma wananchi kwakuwa Corona
huenda ikachukua muda mrefu hivyo kutofanya kazi kutaweza kuleta athari nyingi
mbaya na kubwa ndani ya jamii.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )