DMO KILINDI AWATAKA WAZAZI WANAONYONYESHA KUZINGATIA USAFI KUEPUKA CORONA

 Mganga Mkuu wa wilaya ya Kilindi Mkoani Tanga Daniel ChocholeRAISA SAID,KILINDI.

MGANGA Mkuu wa wilaya ya Kilindi Mkoani Tanga Daniel Chochole amewataka wazazi wilayani hapa wenye watoto chini ya umri wa mitano kuzingatia usafi wakati wa kuwanyonyesha  kwa kuhakikisha wanajenga mazoea ya kunawa mikono na kusafisha matiti ili kujiepusha na maambukizi ya Virusi vya Corona

Aliyasema hayo wakati wa akizungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusu namna wazazi ambao wananyonyesha watoto wao jinsi ya kuchukua tahadhari ya kukabiliana na ugonjwa wa Virusi vya Corona.

Alisema ni vyema wazazi hao kuhakikisha wanakuwa wasafi muda wote ambao wanataka kuwanyonyesha watoto wao wadogo ili kuwaepusha na magonjwa mbalimbali yanayoweza kuwapata.

Mganga huyo wa Wilaya aliwaataka pia wanawake wanaonyonyesha kuhakikisha wanajenga tabia ya kunawa mikono kila wakati ikiwamo kuepuka kukaa kwenye msongamano wa watu wengi.

“Wanawake wanaowanyonyesha watoto wachanga ni vyema wakaepuka kwenda nao kwenye mikusanyiko kwa sababu ni rahisi kwao kupata maambukizi kwa haraka.

“Ni lazima wazazi kuhakikisha wanakuwa wasafi wakati wa kunyonyesha watoto wao hasa kwenye kipindi hiki cha Ugonjwa wa Corona ambao unatikisha Dunia lengo kubwa likiwa kuwaepusha na mambukizi hayo”alisema Chochole.

Aliwataka wazazi kuhakikisha wanawalinda watoto wao wasipate maambukizi ya corona huku wakiepuka kuwapa wageni watoto wao kabla ya kunawa mikono yao .

Awali akizungumza mkazi wa Kwediboma wilayani humo Agnes Charles alisema kwamba wakati huu wa ugonjwa wa Corona wamekuwa wakichukua tahadhari kubwa wakati wanapokuwa wakiwanyonyesha watoto wao hasa kwa kuhakikisha wanakuwa wasafi.

                                                
                           

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )