DKT. NCHIMBI AMPA TANO RAIS KWA KUIINGIZA TZ UCHUMI WA KATI

 Mkuu wa MKoa wa Singida Dkt. Rehema
Nchimbi akifunga  mafunzo maalum ya  siku sita kwa wadau zaidi ya 300
kutoka katika mikoa mbalimbali nchini  yaliyokuwa yameandaliwa na Baraza
la Taifa  la watu wanaoishi na  virusi vya UKIMWI (NACOPHA) kupitia
“Mradi wa Hebu Tuyajenge” unaotekelezwa katika kipindi cha miaka mitano
2019-2024, unaofadhiliwa na  Shirika la Marekani  la  Maendeleo ya
Kimataifa (USAID) katika mikoa 22 Tanzania Bara. kushoto Mkuu wa Wilaya
ya Manyoni Rahabu Mwagisa, Kulia Mkurugenzi wa Utatifi wa NACOPHA 
Pantaleo Shoki

>Awataka wenye virusi kufanya kazi bila hofu

>Awaonya wanaomchokoza,asisitiza hatatia nia

Na John Mapepele 
 
 Mkuu wa
Mkoa wa Singida
, Dkt. Rehema Nchimbi
amempongeza Rais Magufuli kwa kuvunja rekodi ya 
maendeleo kabla ya mwaka 2025 na kuifanya Tanzania kuingia kwenye nchi
za uchumi wa kati duniani Julai Mosi mwaka huu.  
Huku akiwahimiza watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI nchini  kufanya kazi kwa  bidii bila kuwa na hofu sambamba na kumtanguliza Mungu na kutumia fursa za
mikopo inayotolewa na Serikali ya Awamu ya Tano ili  ku kuinua hali za maisha na kuongeza pato la
taifa kwa ujumla

Dkt. Nchimbi ameyasema hayo leo katika Mji Mdogo wa Manyoni mkoani  Singida alipokuwa akifunga  mafunzo maalum ya  siku sita kwa wadau zaidi ya mia 3 kutoka
katika mikoa mbalimbali nchini 
yaliyokuwa yameandaliwa na Baraza la Taifa  la watu wanaoishi na  virusi vya UKIMWI (NACOPHA) kupitia “Mradi wa Hebu Tuyajenge”.
Mradi huo unaotekelezwa katika kipindi cha miaka mitano
2019-2024,unaofadhiliwa  na  Shirika la Marekani  la 
Maendeleo ya Kimataifa (USAID) katika mikoa 22 Tanzania Bara.

Amesema kwa sasa Serikali ya Awamu ya Tano imepiga hatua kubwa ya kupiga
vita unyanyapaa dhidi ya watu wanaishi na virusi vya UKIMWI na kwamba watu wote
wana haki na fursa sawa  mbele ya
Serikali yao hivyo hakuna sababu ya  wao
kuendelea kujinyanyapaa  wenyewe  na badala yake wawe walimu wa kuwaelimisha
wengine kwenda kupima na kutambua hali zao 
na kuendelea kuchapa kazi ili kuinua uchumi wan chi yetu.

“Kubwa ndugu zangu hapa ni 
kumtanguliza  Mungu mbele, kutoa
hofu na  kuachana  na mambo yote ambayo yanapelekea  kudhoofu kwa afya zetu kama vile unywaji wa
pombe  hata kama wake zetu wanapika  kwa ajili ya biashara na badala yake tutumie
juisi lishe za matunda ya asili kama vile 
Sasati, Ubuyu na Ukwaju” amesisitiza Dkt. Nchimbi

Umewaelekeza  Wataalam wa
Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Singida kuangalia namna  ya kuja na mikakati madhubuti ya kiuendelevu
ya kuwakopesha wanaoishi na UKIMWI  ili
kuwaletea maendeleo huku akisisitiza kuwa 
Mkoa wake utaendelea kutekeleza mikakati iliyojiwekea ya kuinua
maisha  ya wanainchi wake ikiwa ni pamoja
na mkakati wa kuwavusha salama mama na mtoto.

Aidha ameweka
msimamo wake wa
kutokuonesha
nia yeyote ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge katika uchaguzi wa mwaka huu
huku akiwaonya
watu ambao wamekuwa wakianza kudanganya kuwa atagombea ambapo
alisisitiza kuwa
nafasi
hiyo ya ukuu wa Mkoa aliyopewa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli ni ya
heshima kubwa.

“Naomba niliseme  hili, na tayari
nimeshalisema mara kadhaa  hata hivi
karibuni nilipokuwa
nyumbani
kwangu, kijijini Matufa
,  Babati Manyara nilipo hudhuria mazishi ya mtoto wa Kaka
yangu ali
yefariki
kwa ajali ya Pikipiki kwamba
nilikwenda kuungana na familia yangu katika msiba wa kijana
wetu na si vinginevyo. Ninaridhika sana na nafasi hii niliyo nayo ya ukuu wa
Mkoa” alisema Dkt. Nchimbi huku akishangiliwa na umati wa  wadau wa mafunzo hayo

Baadhi ya
waombolezaji wamesikika kupongeza msimamo wa kiongozi huyo
, huku wakisema  kuwa Msimamo huo unapaswa kuigwa na viongozi
wengine  kwa kuwa umejikita katika
kuwaletea maendeleo wananchi badala ya kuwa na tamaa za madaraka.

“Binafsi nampongeza sana Mama Nchimbi 
kwani kwa muda wote amekuwa aking’ang’ana na kuwaunganisha watu wote
bila kujali dini wala rangi kwa, hata sisi leo ametutia moyo sana kiasi
kwamba  baada ya kutoka hapa tumekuwa na
nguvu mpya  ya kuchapa kazi na
kushirikiana na Serikali yetu ya 
kujiletea maendeleo Zaidi ili tutoke katika nchi za uchumi wa kati na kwenda
katika nchi tajiri duniani na tuna imani kubwa chini ya Rais wetu Magufuli
tutafika” amesema Amina  Huredi ambaye ni
Mshiriki wa mafunzo hayo kutoka Singida

Mkurugenzi wa Utatifi wa NACOPHA  Pantaleo Shoki  amemshukuru Mkuu wa Mkoa na kumhakikishia
kuwa  wataendelea kushikiana na Serikali
ili kuhakikisha kuwa malengo ya Mradi huo yanatimia kama yalivyopangwa.

Shoki 
amesema Mradi  unalenga kufikia
Mkakati wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na UKIMWI(UNAIDS) wa
95-95-95 yaani  asilimia 95 ya watu wote
wanaoishi na maambukizi ya VVU wawe wamepima na kugundua afya zao,asilimia 95
ya watu wote waliopimwa na kukutwa na maambukizi wawe wameanza tiba na asilimia
95 walio kwenye tiba wawe wamefubaza virusi hivyo ifikapo 2030

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )