DK. MOLLEL ATEMBELEA HOSPITALI YA CCRT JIJINI DAR ES SALAAM LEO

    Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Brenda Msangi akizungumza na Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dk. Godwin Mollel jijini Dar es Salaam leo alipotemelea Hospitali ya
CCRBT.
 Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dk. Godwin Mollel akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa hospitali
ya CCBRT.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Godwin Mollel akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Brenda Msangi alipotemelea katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam leo.
 
NAIBU
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dk. Godwin Mollel, afanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya CCBRT
iliyoko Msasani jijini Dar es Salaam leo.Akizungumza
na wafanyakazi wa Hospitali ya CCBRT, Dk Mollel amesema kuwa anatambua
mchangao wa hospitali hiyo katika kuwahudumia watanzania kwa upande wa
afya.“Nawafahamu
CCBRT na kazi mnazozifanya kwa muda mrefu sasa, nawapongeza kwa kazi
nzuri, kama Serikali tunatambua mchango wa hospitali hii katika
kuwahudumia watanzania, leo nimefika kusalimia kidogo lakini naahidi
kuja rasmi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja ili tuweze kupata wasaa wa
kujadilina kwa kina juu ya kazi zenu”. Amesema Dk. MollelKwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Brenda Msangi

amemshukuru
Dk. Mollel kwa kufika katika Hospitali ya CCBRT, na kumueleza ambavyo
taasisi yake inanufaika na ubia kati yake na serikali tangu kuanza kwake
hadi hapa ilipofikia. “Kwa
niaba ya wafanyakazi wenzangu wa CCBRT napenda kuchukua nafasi hii
kuishukuru Serikali yetu kupitia Wizara ya afya tumekuwa tukipata msaada
na ushirikiano mkubwa  kutoka serikalini kwa hili, nasema asante sana
na naomba utufikishie salam zetu kwa dada yangu Mheshimiwa Ummy Mwalim
na watendaji wake wote”. Amesema BrendaHata hivyo Katika ziara isiyo rasmi Naibu waziri, amekutana na kusalimiana na uongozi wa hospitali hiyo huku akiwapongeza CCBRT kwa kazi nzuri  pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo.

 

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )