DC WA SINGIDA AJA NA OPERESHENI TOKOMEZA CORONA

    Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi
Paskasi Muragili akiwa ndani ya basi la Kampuni ya Kiazi Kitamu akiwaeleza
abiria mbinu za kujikinga na Virusi vya Corona (COVID-19) alipokuwa kwenye
Operesheni maalum ya Tokomeza Corona Katika Manispaa ya Singida kwenye Kituo
Kikuu cha mabasi. (Picha na. Peter Kashindye).
Madereva na Mawakala wa mabasi kwenye
Kituo Kikuu cha mabasi ya Mkoa wa Singida (Misuna) wakionyesha jinsi ya kutumia
vitakasa mikono ili kukabiliana na ugonjwa wa Corona (COVID-19) kwa Mkuu wa Wilaya
ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili (Hayupo pichani) alipofanya Operesheni Maalum
ya Tokomeza Corona Katika Manispaa ya Singida kuona utekelezaji wa maagizo ya
Serikali ya kujikinga na ugonjwa huo (Picha na. Peter Kashindye).  Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi
Muragili (aliyenyanyua mkono) akihoji uelewa wa kujikinga na virusi vya Corona
(Covid-19) mahali pa kazi kwenye maduka ya kuuzia nyama alipofanya Operesheni Maalum
ya Tokomeza Corona Katika Manispaa ya Singida kwenye Soko Kuu la Singida Mjini.
(Picha na. Peter Kashindye).

1.  Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi
Paskasi Muragili akiwasisitiza wafanyabiashara wadogo juu ya matumizi sahihi ya
vitakasa mikono alipofanya Operesheni maalum ya Tokomeza Corona Katika Manispaa
ya Singida kwenye Soko Kuu la Singida Mjini. (Picha na. Peter Kashindye).1  Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi
Muragili (aliyenyanyua mkono) akitoa maelekezo kwa madereva na mawakala
kuzingatia miongozo iliyotolewa na Wizara ya Afya juu ya kujikinga na
maambukizi ya virusi vya Corona (Covid-19). (Picha na. Peter Kashindye).

Na John Mapepele ,Singida

Mkuu wa Wilaya ya Singida Injinia
Paskasi Damian Muragili amefanya Operesheni Maalum kwenye maeneo
mbalimbali ya Mji wa Singida kutoa elimu na kuona jinsi wananchi
walivyotekeleza maelekezo ya Serikali kuhusu ya kujikinga na ugonjwa
unaoambukizwa na Virusi vya Corona (Covid 19).

Licha
ya kutoa elimu hiyo pia amewapiga faini za hapo hapo watu waliobainika
kukiuka maagizo huku akisisitiza kuwa Serikali itawanyang’anya lesseni
za biashara na kufunga biashara hizo wote ambao wataendelea kukaidi
maelekezo hayo
 

Mhandisi
Muragili amefanya Operesheni hiyo maalum akiwa na Kikosi Kazi cha
wataalam mbalimbali kwenye Wilaya yake ambapo ilianza alfaji hadi usiku
wa kuamkia leo ambapo alitembelea maeneo yote ya huduma katika Mji wa
Singida iliyojumuisha maeneo ya Standi Kuu ya Mkoa wa Singida ya Misuna,
Soko Kuu la Singida na maeneo ya biashara ya Bajaji.

Akiwa
katika Soko Kuu la Singida, Mkuu wa Wilaya alifanikiwa kukuta maduka ya
nguo ya Kikundi cha Ushonaji cha Singida yakiwa hayana vitakasa mikono
lakini wauzaji walikuwa wakiendelea na shughuli za biashara na kuwatoza
faini ya shilingi elfu 50 papo hapo.

Akilipa faini hiyo baada ya
kukiri kosa hilo, Mwenyekiti wa kikundi hicho ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Mtaa wa Soko Kuu Singida Amina Msaghaa aliomba samahani kwa Mkuu wa
Wilaya na kuahidi kutoendelea kufanya kosa hilo na kwamba faini hiyo
imekuwa fundisho kwao na kwa hiyo wao kama kikundi watakuwa mfano wa
kuwafundisha wafanyabiashara wengini

“Mhe. Mkuu wa Wilaya
naomba kukueleza kuwa tumetoa faini hii kwa masikitiko makubwa, lakini
hii inatupa ujasiri wa kushirikiana na Serikali yetu kuhamasisha kuhusu
kujikinga na ugonjwa huu, naahidi tutakuwa walimu wazuri” alisitiza
Msaghaa

Mwenyekiti wa Waendesha Bajaji Mkoa wa Singida Hemed
Juma amesema katika kupambana na ugonjwa wa Corona chama chao
kimechukua tahadhari zote zinazoelekezwa na Serikali kuhusu ugonjwa huu
na kwamba yoyote atakayekaidi atashughulikiwa kikamilifu na chama chao
ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwenye Vyombo vya Sheria.

Akifanya
ukaguzi kwenye mabasi yanayoingia na kutoka kwenye Stendi Kuu Mkuu
wa Wilaya amesema abiria wanatakiwa kutumia vitakasa mikono
wanapoingia na kutoka kwenye mabasi hayo kwa ajili ya kujikinga na
ugonjwa huu

Aidha amesema Operesheni hiyo imeanza na itakuwa endelevu na ya kushitukiza kila wakati hadi ugonjwa huu utakapoisha.

Amewataka
kila mwananchi wa Wilaya ya Singida kuwa mzalendo kwa kuzingingatia
maelekezo ya Wizara ya Afya ya kujikinga na ugonjwa huu kwa kujitenga na
kuchukua hatua zinazotakiwa ili kujilinda na kuwalinda wengine na
kwamba wanapohisi kuwa kuna mgeni ambaye ameingia na hajapimwa watoe
taarifa kwenye Mamlaka zilizo katika maeneo yao

Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt Rehema Nchimbi katika siku za hivi karibuni ameanza ziara
maalum ya kuhamasisha wananchi wa mkoa wake kuchukua tahadhari za
kujikinga na ugonjwa huu kwa kufuata taratibu zote zinazotolewa na
wataalam wa afya za kudhibiti na kujikinga na ugonjwa, wa Covid-19,
kumwomba Mungu na kuendelea kuchapa kazi ili kunusuru kupoteza maisha na
kushuka kwa uchumi wa nchi yao

Akiwa kwenye Soko maarufu la
viazi lishe kwenye Kitongoji cha Kideka katika Kijiji cha Nkunikana
aliwapongeza wafanyabiashara hao kwa kuzingatia maelekezo ya Serikali ya
kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 kwa kuandaa miundombinu
ya maji ili kunawa mikono kwa sabuni katika maji yanayotiririka
wakati wote.

Aidha 
aliwataka wakulima wa viazi lishe kuendelea kulima kwa bidii ili
wananchi wapate lishe bora kutokana na viazi hivyo na majani yake ambapo
alisisitiza kuwa katika kipindi hiki ni muhimu kusanitaizi mikono na
kusanitaizi afya zao

“Naelekeza wakulima waache visingizio nao
waendelee kwenda mashambani kujitenga na kulima kwa bidii katika kipindi
hiki ili waweze kupata mazao mengi na wakati huo huo watekeleze matakwa
ya Serikali ya kujitenga na mikusanyiko isiyo ya lazima ambayo ingeweza
kusababishia maambukizi endapo mmoja ana maambukizi.”

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )