DC Morogoro atoa siku 14 wenye vibanda vya nyasi kuondoka Msamvu.

Mji wa Morogoro umekumbwa
na taharuki usiku wa kuamkia juzi baada ya moto kuzuka katika stendi kuu ya
mabasi Msamvu na kuteketeza vibanda vya wafanyabiashara wanaoendesha shughuli
zao katika stendi hiyo, ambapo Mkuu wa wilaya ya Morogoro Regina Chonjo, ametoa
agizo la siku 14 kubomolewa kwa vibanda vyote vilivyopo kituoni hapo.
Mkuu wa wilaya ya Morogoro ameeleza hayo baada ya tukio la
moto uliosababishwa na uunguwaji holela wa umeme katika vibanda hivyo na
kusababisha kuteketeza mali zao. Zaidi ya vibanda viwili huku Mkuu wa Wilaya
akimuagiza meneja wa tanesco morogoro kukata umeme unaongia katika vibanda
hivyo.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )