CORONA ITAPITA TANZANIA ITABAKI KAMWE MSITISHWE.

 

Tupo vitani!Dunia ipo vitani, Afrika ipo vitani na Tanzania IPO vitani dhidi ya adui Corona.

Majeshi yanapoingia kwenye Vita kila jeshi utumia mbinu zake kushinda Vita Wala hakuna”Standardised war plan” ya kuweza kumshinda adui wako.

Kushinda adui ukiwa vitani inategemea mambo mengi lakini Jambo la muhimu kabisa ni uwezo wa makamanda wako “kumaneuver” wakiwa katika Uwanja wa vita.

Kamwe tusimpangie Kamanda Mkuu jinsi gani apigane Vita dhidi ya Corona kwa maana ata wimbi la kwanza la Corona lilivyokuja watu walipiga kelele sana lakini yeye alijua nini anachofanya.

Serikali kupitia kwa Msemaji Mkuu wake ilishasema kwamba Corona IPO na sio ipo Tanzania tu Corona IPO dunia nzima kwahiyo tunapaswa kuchukua tahadhari kwa kufwata maelekezo ya Wizara ya afya pamoja na kumuomba Mungu.

Maelekezo ya Serikali kupitia Wizara ya afya yapo wazi kabisa kwa maana matumizi ya tiba asili ili kujenga kinga ya mwili,hakuna zaidi ya hapo!sasa mnataka Rais aseme nini?

Lazima tuelewe kuwa tupo vitani na kama kuna mtu atashangaa vifo wakati wa Vita tutamshangaa yeye.

Ni kama kuna kakikundi ka watu fulani kanafurahia hii hali ya vifo katika Taifa lakini kibaya zaidi wanataka kumtupia lawama Rais Magufuli lakini sijui lawama hizo ni kwa lipi?

Lazima Watanzania tuukatae “ushetani” huu kwa nguvu zote,tabia ya kusherekea vifo katika Taifa hili imeanza lini?,hivi Wapinzani wamekosa ajenda za maana mpaka wanaanza kutumia vifo kupata “Popularity”?

Tupo vitani kwahiyo vifo lazima vitatokea kamwe Watanzania MSITISHWE,Wala hatutakufa wote lakini tukubali kuwa tutaendelea kupokea habari za vifo dhidi ya wapendwa wetu lakini twapaswa kuwa na subira.

Nchini Kenya zaidi ya watu maarufu watano wamefariki ndani ya siku sita,Nchini Zimbabwe zaidi ya Mawaziri wanne wamefariki mwezi huu na maeneo mengi mengine duniani. 

Sisi nani mpaka tusiguswe na wimbi hili?tunasema Mungu aliyetuponya mara ya kwanza ndio huyo huyo atatuponya kwa mara nyingine,Watanzania wawe watulivu kwani Corona itapita kama ambavyo wimbi la kwanza la ugonjwa wa Corona lilivyopita.

Kamwe huu sio mwisho wa dunia,mtanzania chukua tahadhari zote za kiafya na zidisha katika kumuomba Mungu atuponye na vifo hivi.

Pole Mh Rais,pole kwa Watanzania wote lakini Corona itapita na Tanzania itabaki hakuna sababu ya kutishana!Jilinde!

WILLIUM PETER NDILLA

SUMVE, KWIMBA.

+255 759 929244

February 18,2021.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )