CCM UBUNGO YAMPONGEZA DC MAKORI KWA UTENDAJI

 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori, (kushoto) akiwasilisha taarifa
yake mbele ya Kamati ya Siasa Wilaya ya Ubungo, katikati ni Mwenyekiti
wa CCM wa Wilaya  ya Ubungo, Lucas Mgonja pamoja na Katibu wa wilaya
hiyo, Chifu Silvester Yaredi

Wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Ubungo, wakijadili taarifa ya utendaji ya Mkuu wa Wilaya
Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM
 
KAMATI ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ubungo,
chini ya mwenyekiti wake Lucas Mgonja, imempongeza Mkuu wa Wilaya ya
Ubungo, Kisare Makori kwa utendaji wake ikiwamo vita dhidi ya ugonjwa wa
corona wilayani humo.


Taarifa ilitolewa leo na Katibu wa Siasa ya Uenezi, Wilaya
ya Ubungo, Mbaruku Masudi, imeeleza kuwa katika kikao hicho pamoja na
mambo kilipokea taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori 
ikiwamo hali ya ugonjwa wa corona, ujenzi wa vyumba vya madarasa na
matundu ya vyoo kwa shule za msingi na sekondari wilayani Ubungo.


“Jana tarehe 6/05/2020  Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu
ya CCM Wilaya ya Ubungo ilikuwa na kikao chake cha kwanza cha kawaida
kwa mwaka 2020.


“Katika Kikao hicho pamoja na mambo mengine kilipokea
taarifa kutoka kwa Kamisaa wa chama Mkuu wa Wilaya Kisare Makori ikiwamo
taarifa ya hali ya ugonjwa wa corona katika wilaya yetu (Ubungo) na
jitihada zinazofanyika.


“Ujenzi wa vyumba vya madarasa, ofisi za walimu, matundu ya
vyoo na ununuzi wa viti, meza na madawati. Pia kikao kilijadili hali ya
uharibifu wa miundombinu ya barabara nahatua zilizochukuliwa hasa
katika kipindi hicho cha mvua,” amesema Mbaruku


Katibu huyo Mwenezi wa Wilaya ya Ubungo, amesema kuwa
pamoja na hali hiyo pia walipokea taarifa ya kutoka kwa DC Makori kuhusu
kupatikana kwa eneo la ujenzi wa mahakama ya wilaya, polisi, Zimamoto
na Uokoaji pamoja na ujenzi wa ofisi ya Katibu Tarafa Kibamba eneo lenye
ukubwa wa takribani ekari 11.9.


“Pia Kamati ya Siasa ya Wilaya chini ya Mwenyekiti Mgonja
ilipokea taarifa kuhusu suala la bei elekezi ya sukari na hatua
zilizochukuliwa,” amesema


Kutokana na hali hiyo amesema kuwa CCM Wilaya ya Ubungo,
kimeipongeza Serikali ngazi ya wilaya na kuishauri kuongeza jitihada
katika kutoa elimu kuhusu kingi dhidi ya ugonjwa wa corona ikiwamo
kujilinda na janga hilo.


Pamoja na hali hiyo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo,
Lucas Mgonja, alitoa wito kwa wana CCM kuendelea kushirikiana na
Serikali katika kipindi hiki ili kuhakikisha maelekezo yote muhimu
yanatolewa yanazingatiwa.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )