BURIANI MNYARIGUSU ASHA MUHAJI

Katika darasa letu la TSJ (2004-2006) Alumni Asha Muhaji (picha ya chini aliyechuchumaa mbele kulia) ulikuwa malenga wetu wa Kiswahili. Uliiweza lugha yetu adhimu kinyumenyume. Umahiri ambao ulitamba nao katika newsroom zote ulizopita. 
Sikumbuki jina lilianzia wapi ila kila mtu darasani aliitwa Mnyarugusu. Nalia kwani kusikia kifo chako nimemkumbuka Mnyarugusu Farida Kipingu aliyetangulia mbele ya haki muda si mrefu baada ya kuhitimu TSJ. 
Busara na ucheshi wako vilikufanya uwe daraja muhimu wakati na baada ya chuo. Uliongoza mitoko yote ya darasa, hata kule Mikadi beach ulikuwepo kuwapa moyo wanyarugusu waliokwama majini. 

Miezi kadhaa iliyopita ulikuwa unahangaikia Get together ya wanyarugusu. Nalia kwa kumaizi kwamba tutakutana msibani kwako tukiwa na majonzi. 
Tusalimie Farida Kipingu na Iddi Kikuzi, Mwalimu Kayuza na wengineo. Usimsahau kaka yetu kipenzi Baba Mbelwa. Waambie tunawa-miss kichizi. InshaAllah iko siku tutakutana huko mliko kwani ni njia yetu sote. 
PUMZIKA KWA AMANI ASHA


Inna Lillahi wa inna ilayhi raji’un

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )