BODI YA MAZIWA YAINGIA MAKUBALIANO YA UNYWAJI MAZIWA MASHULENI

 

Jane Edward, Msumba News, Arusha

Shule 13 za msingi mkoani Arusha zimetia sahini  na Bodi ya maziwa Tanzania ya makubaliano ya utekelezaji wa mpango wa  unywaji wa maziwa shuleni .

Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini makubaliano hayo Kaimu  msajili Bodi ya maziwa nchini Noely byamungu  amesema lengo la mpango huo Ni kutekeleza maagizo yaliyotolewa na serikali na kwa Arusha mpango huo  ulianza January 14 .

Awali mgeni rasmi katika hafla hiyo kaimu katibu tawala mkoa wa Arusha devid lyamongi  akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa ameishukuru Bodi ya maziwa kwa kuitikia mwitikio wa serikali ya uanzishwaji mpango wa unywaji wa maziwa shuleni kwa mkoa wa Arusha

Nae mwanasheria wa bodi ya maziwa Edwin amesema  Bodi hiyo imekubaliana na kiwanda  Galax food and a beverage ltd kuuza maziwa shuleni na shule walizoanza nazo Ni 13 na wanategemea unywaji wa maziwa utaongezeka kwa mwaka huu kuliko miaka mwingine.

Hata hivyo mpango huo wa unywaji maziwa katika shule hizo unatajwa utaongeza weledi na ufaulu kwa wanafunzi.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )