BMU ZAPANDISHA MAPATO HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI

 

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya
ya Pangani, Issaya Mbeje katikati akiteta jambo wakati wa ziara ya

ujumbe wa vikundi vya BMU kutoka
katika halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo uliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa
halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo Chandika Dismas Chandika pamoja na Mwenyekiti
ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira katika ziara ya siku moja ambayo imedhaminiwa
kupitia mradi wa SWIOFish Tanzania bara kushoto ni

Amina Kiaratu ambaye
kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Uvuvi pia ni Afisa Mawasiliano
kwenye Mradi wa Swiofish Tanzania Bara
Amina
Kiaratu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Uvuvi ambaye pia ni
Afisa Mawasiliano kwenye Mradi wa Swiofish Tanzania Bara akizungumza
jambo wakati wa ziara hiyo kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya
ya Pangani Isaya Mbenje

  • Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Chandika Dismas Chandika akizungumza wakati wa ziara hiyo
AFISA Uvuvi wa  Mradi wa Swiofish wilaya ya Bagamoyo Yasinta Magesa akizungumza wakati wa ziara hiyo

Wajumbe wa BMU wilaya ya Bagamoyo wakiwa kwenye soko la Kipumbwi wilayani Pangani wakati wa ziara yao ya mafunzo

Wajumbe wa BMU wilaya ya Bagamoyo wakiwa kwenye soko la Kipumbwi wilayani Pangani wakati wa ziara yao ya mafunzo

Wajumbe wa BMU wilaya ya Bagamoyo wakiwa kwenye soko la Kipumbwi wilayani Pangani wakati wa ziara yao ya mafunzo

Jengo la BMU Kata ya Kipumbwi wilayani Pangani

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya
ya Pangani, Issaya Mbeje amesema kuwa siri ya halmashauri hiyo kupaa kimapato
katika makusanyo ya ushuru wa mazao ya bahari ni kutokana na kutumia vikundi
shirikishi vya usimamizi wa rasilimali za uvuvi(BMU).

Vikundi
Shirikishi vya Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi(BMU) halmashauri ya wilaya ya
Pangani vilianzishwa kupitia mradi wa MACEMP mwaka 2009 na utendaji wake
unazingatia Sera ya Uvuvi ya sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 na Mwongozo
wa kitaifa wa BMU wa mwaka 2005.

Mbenje
amebainisha hayo katika ofisini kwake kwa ujumbe wa vikundi vya BMU kutoka
katika halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo uliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa
halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo Chandika Dismas Chandika pamoja na Mwenyekiti
ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira katika ziara ya siku moja ambayo imedhaminiwa
kupitia mradi wa SWIOFish Tanzania bara unaofadhiliwa na Benki ya Dunia(WB).

Mbali na
Tanzania mradi wa SWIOFish pia unatekelezwa katika nchi za Msumbiji na Commoro.

Amesema
kuwa wilayani humo maeneo manne ambao vikundi hivyo vinafanya kazi katika
vijiji 12 katika ukanda ambavyo ni Mkwaja,Kipumbwi,Pangani Mashariki na Pangani
Magharibi.

Amebainisha
kuwa katika mwaka wa fedha 2014/15 BMU ilipoanzishwa walifanikiwa kukusanya
fedha kiasi cha Sh.23.8 milioni,mwaka 2016 walikusanya Sh.35,517,290/-,mwaka
2016/17 walikusanya Sh.128,178.567/-na mwaka 2017/18 mapato yalipanda hadi
kufikia Sh.256.8 milioni.

Alisema
kuwa katika mwaka wa fedha 2018/19 baraza la madiwani katika halmashauri hiyo
waliamua kuwapa kazi ya kukusanya mapato maafisa watendaji wa vijiji ambapo
walifanikiwa kukusanya Sh.162.051,600/- na mwaka 2019/20 mapato yalishuka na
kukusanya Sh.137,354,125/-.

“Katika miaka
ya nyuma wakati tuanaanza kukusanya mapato ya mazao ya bahari tuliwatumia BMU
mapato yalipanda sana lakini walipopewa watendaji wa vijiji mapato
yalishuka,hivyo baadae baraza la madiwani likaona bora tuwatumie tena BMU ambao
wanafanya kazi kupitia serikali za vijiji husika,hivyo tumezifufua na
kuwajengea uwezo,kuwapa mafunzo ya kukusanya mapato kupitia shirika la
SeaSense,”.

 “Baada ya baraza la madiwani kufanya mapitio ya bajeti kuona mapato
yanashuka,kamati ya fedha tulibainia mapungufu na kupitia upya mikataba ya BMU
tukaona tuwape kazi ya kukusanya mapato ya mazao ya bahari ambapo katika
kipindi cha kuanzia July 1 2020 hadi January 2021 tumeafanikiwa kukusanya Sh.93
milioni. Na BMU wakishakusanya mapato tunawapa kamisheni ya asilimia 10”.Alisema

Mwenyekiti
wa BMU Pangani Magharibi  John Frank Baya
alisema kuwa safari ya kuanza kukusanya mapato ilianza mwaka 2014 kwa majaribio
ya muda wa miezi 6 walifanya vizuri ndipo baraza la madiwani wakaona wawape
kazi hiyo kabla ya baadae kuwapa watendaji wa vijiji kisha kuwarudisha tena.

Alifafanua
kuwa siri kubwa ya mafanikio ya BMU katika kukusanya mapato ni kushirikisha
wajumbe wote wa pamoja na kutoa elimu katika jamii ya kijiji katika kukusanya
mapato ambapo wa natoa ushirikiano kutoka katika asilimia 10
wanayopata,asilimia 5 wanairudisha kijijini ambapo inasaidia kuduma za jamii.

“Tunapokusanya
ushuru tunashirikisha jamii katika kijiji husika pamoja wajumbe wote wa BMU na
kutoa elimu hivyo hawakwepi ushuru na wavuvi wenyewe tunawaelimisha faida ya
ushuru ambapo pia unawasaidia wenyewe na wanatuelewa,”alisema.

Makamu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo amsema kuwa kupitia BMU za
Pangani wamefurahishwa na jinsi halmashauri hiyo ilivyoweza kufanikiwa
kukusanya mapato ya mazao ya bahari kupitia BMU na kuahidi kuenda kutoa elimu
kwa madiwani wa Bagamoyo na BMU katika kukusanya mapato katika rasilimali za
bahari.

Kwa
upande Adhri Mohamedi  mvuvi katika eneo
la Kipumbwi amebainisha faida wanazozipata kupitia BMU ni pamoja na kupewa
msaada pindi wanapopata majanga.

“Tunapotoa
mapato  faida nyingine inarudi kwetu,kwa
mfano hivi karibuni kuna mvuvi mwenzetu alipotea lakini tulitoa taarifa BMU
walitusaida fedha na mafuta hadi tukafanikiwa kumpata,”alisema

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )